Kufuatia
matoleo ya simu mbalimbali yiliyotangulia, TECNO, imekua ikitajwa tajwa huku
ikihusishwa na ujio wa toleo jipya ikikisiwa kuwa ni muendelezo wa matoleo ya
Camon, ni ukweli usiopingika kuwa matoleo ya TECNO-Camon yamekua na kamera
nzuri zaidi kufananishwa na matoleo mengine
Miongoni mwa vivutizi vinavyoipa simu kipaumbele, bila shaka
simu inatakiwa iwe na kamera yenye megapixel kubwa, TECNO, wamelizingatia hilo
Baadhi ya kurasa za mitandaoni zimeihusisha kampuni ya TECNO
juu ya ujio wa toleo jipya likipewa jina la Camon kufuatia histoia ya kampuni
kuzindua Camon CX mwaka jana miezi kama hii, bado hakujawa na uhakika wa taaifa
hizi hivyo ni propaganda tu
Simu
hiyo inakadiriwa kuwa na megapixel 16 mbele pamoja na flashi maalum kwa picha
za ‘’selfie’’, uwezo wa kupiga picha zenye ubora wa HD, kamera yake ya nyuma
kuja na megapixel nyingi zaidi ssambamba na flashi maalum zinaakisi mwanga ili
kupata kuendana na mazingira.
Maswali kuhusiana na ujio wa simu hiyo `yamekua mengi sana
pasina kupata majibu yenye uhakika, kamera inayoweza kupiga picha nyingi ndani
ya mfupi zikiwa na ubora wa HD?, bado inaniacha na maswali yanayoamsha morali
ya kutaka kujua zaidi
Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti http//www.tecno-mobile.com
0 Comments