Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Mambo ya
nje, ulinzi na usalama wakikagua Mradi kuhusu Tathmini na ulipaji wa fidia ya
Ardhi, kilwa Navy Military Base katika tukio lililofanyika wilayani kilwa
Mkoani Lindi.
Mkuu wa kitengo cha usimamizi na Maendeleo ya
Miliki kutoka Wizara ya ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, Ndg. Sebastian Bebwa
akiwapa maelezo mafupi Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Mambo ya nje, ulinzi
na usalama kabla ya kwenda kukagua Mradi kuhusu Tathmini na ulipaji wa fidia ya
Ardhi, kilwa Navy Military Base katika tukio lililofanyika wilayani kilwa
Mkoani Lindi.
Mkuu wa kamandi ya Wanamaji, Meja Jenerali
Richard Mtayoba akiwapa maelezo Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Mambo
ya nje, ulinzi na usalama wakati alipoenda kukagua Mradi kuhusu Tathmini na
ulipaji wa fidia ya Ardhi, kilwa Navy Military Base katika tukio lililofanyika
wilayani kilwa Mkoani Lindi.
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Mambo
ya nje, ulinzi na usalama, Mhe. Mussa Zungu akizungumza na Wajumbe wa kamati
hiyo, watendaji wakuu toka wizarani, ngome, kamandi ya wanamaji na halmashauri
ya wilaya ya kilwa wakati kupokea na kujadili taarifa ya Wizara ya ulinzi na
Jeshi la kujenga Taifa iliyofanyika Wilayani kilwa Mkoani Lindi. Kulia ni
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi, kushoto
ni Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Salum Rehani na wa pili kushoto ni Mkuu
wa kamandi ya Wanamaji, Meja Jenerali Richard Mtayoba
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe.
Dkt. Hussein Mwinyi akizungumza na Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya
Mambo ya nje, ulinzi na usalama wakati wa kupokea na kujadili taarifa ya Wizara
ya ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa iliyofanyika Wilayani kilwa Mkoani Lindi. kushoto
ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Mussa Zungu, Makamu Mwenyekiti Mhe. Salum
Rehani (wa pili kushoto) na kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi
la Kujenga Taifa, Dkt. Florence Turuka.
(PICHA
NA OFISI YA BUNGE)



0 Comments