Makamu Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi na Madawa ya
kulevya, Mhe. Dkt. Jasmine Tiisekwa Bunga (aliesimama)akizungumza na wana konga
wanaoishi na VVU katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, Mkoa wa Songwe pale
kamati hiyo ilipotembelea konga hiyo kwa ajili ya kuamasisha utumiaji wa dawa na
jinsi ya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU).
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Capt. Chiku Galawa
(kulia) akizungumza na Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Masuala ya
Ukimwi na Madawa ya kulevya, Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na VVU (NACOPHA)
pamoja na JSI, iliyoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Dkt. Jasmine
Tiisekwa Bunga (wa pili kushoto) kabla ya kuanza ziara ya kikazi ya kutembelea
konga ya watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (VVU) katika Halmashauri ya Wilaya
ya Mbozi, Mkoa wa Songwe.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Capt. Chiku Galawa
(kulia) akizungumza na Mjumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi
na Madawa ya kulevya, Mhe. Venance Mwamoto (kushoto) na Makamu Mwenyekiti wa
kamati hiyo, Mhe. Dkt. Jasmine Tisekwa Bunga (katikati) pale kamati hiyo
ilipomtembelea ofisini kwake kabla ya kuanza ziara ya kikazi ya kutembelea
konga ya watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (VVU) katika Halmashauri ya Wilaya
ya Mbozi, Mkoa wa Songwe.
Mjumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Masuala
ya Ukimwi na Madawa ya kulevya, Mhe.Zaynab Vulu (kulia) akisalimiana na wana
konga ya watu wanaoishi na VVU katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, Mkoa wa
Songwe pale kamati hiyo ilipowatembelea katika ziara yake ya kikazi.
(PICHA
NA OFISI YA BUNGE)


0 Comments