Machi 24, 2018, waziri mwenye dhamana na wizara ya nishati
ndugu Dr. Medard Kalemani (MB),
ametembelea kiwanda kipya cha kutengeneza mita za umeme kiitwacho Baobab
Energy Sytems Tanzania, kilichopo eneo la mbezi juu Dar es salaam,
kinachomilikiwa na watanzania.
Akizungumza katika uzinduzi huo, mheshimiwa
waziri amesifu uwekezaji uliofanywa na watanzania hawa, na kueleza wazi kwamba
hiki ni kiwanda cha kwanza chenye teknolojia chanya inayolenga kusaidia
tanzania kuokoa gharama za manunuzi ya mita na vifaa vya umeme kutoka nje ya
nchi.
Katika maeleze yake, mheshimiwa Dr.Medard
Kalemani(MB). Waziri ameipa Tanesco miezi 3 kuhakikisha wanasitisha
ununuzi wa mita za umeme kutoka nje ya nchi kwani tayari viwanda vya ndani
kikiwamo Baobab vimeonesha kuwa na uwezo wa kuzalisha kukidhi mahitaji ya
nchi.
“kwa sasa kiwanda kinauwezo wa kuzalisha mita za umeme elfu thelathini na
nane(38000) kwa mwezi, wakati mahitaji ya tanesco ni mita elfu ishirini kwa
mwezi (20000), hivyo naipa tanesco miezi mitatu waangalie kazi inayofanywa na
wataalamu hawa na waanze kununua mita hizo kutoka kwa wazalishaji hawa wa ndani”.
Kwa sasa nchini tanzania kuna viwanda viwili vya uzalishaji wa mita za umeme,
Baoba ikiwa ni kiwanda kimoja wapo
Pia mheshimiwa waziri ameiagiza tanesco kushirikiana na
wazalishaji hawa wa mita za umeme ili kupunguza ulazima wa kupeleka mita na
vifaa kama hivi nje ya nchi kwaajili ya matengenezo pindi vinapo haribika.
Mkurugezi mkuu wa Baobab Energy Systems Tanzania ndugu, Eng.Hashim Ibrahim amesema
kwamba wamewekeza katika uzalishaji huu wa mita za umeme, kwani wameona
changamoto kubwa serikali iyopata kuagiza mita kutoka nchi nyingine, jambo
ambalo linapelekea uhaba wa
Mita hizi zinazozalishwa nchini zina ubora wa kipekee unaoweza
kutambua mwizi wa umeme, upotevu wa umeme na pia zinapatkana kwa gharama nafuu
zaidi ukilinganisha na gharama ambazo kwa sasa zinatumika kununua mita hizi.
Mkurugenzi mkuu wa Baobab Energy Systems Tanzania ndugu Eng.
Hashim ibrahim ameahidi kwamba kiwanda hichi kimelenga kutoa ajira kwa
vijana wa kitanzania hasa wanaohitimu vyo mbalimbali hapa nchini vikiwamo veta.
Pia ameeleza kwamba malengo mapana ya uanzishaji wa kiwanda hichi pia ni
kusaidia jitihada za mheshimiwa rais wa awamu ya tano Mheshimiwa John Pombe
Magufuli kwenye sera yake ya uwekezaji wa viwanda.



0 Comments