Pichani
kuanzia Kushoto kwenda Kulia ni Charles Kie, Mkurugenzi Mtendaji wa, Ecobank
Nigeria Ltd; Serigne Dioum, Mtendaji wa MTN’s , Hudma za kifedha kwa njia ya mtandao;
Ade Ayeyemi, Ofisa Mtendaji Mkuu wa, Ecobank Transnational Incorporated (ETI),
Rob Shuter, Ofisa Mtendaji mkuu wa MTN na Patrick Akinwuntan, Mtendaji wa Ecobank Transnational Incorporated (ETI)
Na Mwandishi wetu
KAMPUNI ya simu MTN imeingia
ubia na moja ya benki inayoongoza barani Afrika ya Ecobank Transnational
Incorporated (ETI) kuwezesha wateja wao
kufaidika na huduma za kifedha zinazotolewa na makampuni hayo.
Imeelezwa kuwa MTN
ikijivunia idadi kubwa ya wateja wanaotumia huduma zake mbalimbali; mtandao
mkubwa wenye uhakika; bidhaa zenye ubunifu na huduma zake za kifedha kwa
mtandao imeungana na Ecobank kuwezesha wateja wao kuanzisha kufungua akaunti na
kupitisha miamala yao kupitia mtandao wa MTN.
Makampuni hayo mawili
maarufu barani Afrika yametiliana saini mkataba wa makubaliano utakaowezesha
kushirikiana katika kubuni na kuwezesha huduma za kifedha zenye ubora wa
kiwango cha juu kati ya benki hiyo na mtandao wa simu wa MTN.
Miongoni mwa huduma
zitakazotolewa ni kuwezesha miamala mbalimbali kufanyika kwa kutumia simu na
akaunti za benki.
Kutumia mitaji iliyopo
katika uwekezaji ndani ya Ecobank na MTN
kuwezesha miamala ya kimataifa kufanyika kidigitali.
Aidha makubaliano hayo
yatachochea ubunifu wa bidhaa mbalimbali katika upande wa hifadhi ya fedha kwa
njia ya mtandao na ukopeshaji wake na kutoa nafasi ya malipo kwa njia ya
mtandao kwa wateja, wafanyabiashara na mashirika mbalimbali.
Ade Ayeyemi, Ofisa Mtendaji
Mkuu wa Ecobank anasema: “ Mabadiliko ya kidigitali katika mifumo ya benki na
simu kunatengeneza fursa za namna bora ya kuwezesha kutoa huduma za kifedha.
Afrika inalazimika kwenda mbio katika
digiti ili kuwezesha fursa zilizopo zitumike kuwatumikia wateja. MTN na Ecobank leo wamechukua hatua kubwa kuwezesha
fursa hizo” .
Pia alisema kwamba mkakati wa benk hiyo wa kidigiti kwa muda
mrefuj umelenga kuhakikisha nafuu ya uwezeshaji wa miamala katika soko.
Akizungumzia ushirikiano huo
Ofisa Mtendaji Mkuu na Rais, Rob Shuter alisema: “Ushirikiano kati ya mabenki
na watoaji wa huduma za miamala kwa njia ya simu ni muhimu, hivyo uhusiano wetu
wa muda mrefu na Ecobank umelenga
kuwezesha huduma za fedha kuwafikia wananchi wengi na kwa urahisi zaidi.
Tumefurahishwa na maafikiano haya kwani
yametupeleka hatua nyingine, kwani ushirikiano wetu utawezesha ubunifu
utakaowezesha huduma za fedha kupenya kila mahali katika bara hili.”

0 Comments