Kamanda wa polisi Mkoani Pwani,(
ACP )Jonathan Shanna akionyesha silaha na vitu mbalimbali ,ikiwemo
silaha ya kivita inayokaa na risasi 30 kwa wakati mmoja ,ambazo
walizikamata katika gari walilolitumia majambazi waliofanya tukio la
ujambazi wilayani Kisarawe .(Picha na Mwamvua Mwinyi)
Kamanda wa polisi Mkoani Pwani,( ACP )Jonathan Shanna akionyesha gari
lililotumika kufanya ujambazi Kisarawe likiwa na plate no.bandia za
kibalozi huku akiwa ameshika plate no.halisi zilizokuwa zimewekwa ndani
ya gari hiyo .(picha na Mwamvua Mwinyi)
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama Mkoani Pwani ambae pia ni mkuu
wa Mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo ,akizungumzia tukio la
ujambazi lililotokea Kisarawe na kudai Mkoa umejipanga kudhibiti wale
wasioutakia mema Mkoa huo.
(Picha na Mwamvua Mwinyi)
Na Mwamvua Mwinyi,Kisarawe
MAJAMBAZI
wanne wamefariki dunia baada ya kujibizana risasi na askari polisi
,wakati wakijaribu kufanya tukio la ujambazi katika nyumba ya mama
Juliana Shirinde ambae ni mhasibu wa kikundi cha vikoba
Ushelisheli,wilayani Kisarawe.
Aidha
jeshi la polisi Mkoani Pwani,limenasa gari ndogo yenye namba za ubalozi
ambayo waliiweka namba bandia T.17 CD 220 na kuifanyia ujambazi .
Akitoa
taarifa ya tukio hilo ,kamanda wa polisi Mkoani humo, ( ACP) Jonathan
Shanna ,alisema tukio hilo limetokea april 20 asubuhi saa 1:30 ,eneo la
Kibaoni wilayani hapo.
Alieleza
majambazi hayo yanasadikiwa yalikuwa matano wakitumia gari hilo,ambapo
mmoja wao alishambuliwa risasi lakini alifanikiwa kutoweka .
Hata kamanda Shanna, alimtaka jambazi alietoweka kujisalimisha ndani ya masaa 24 .
Alieleza
zipo tetesi zinazodaiwa baadhi ya waganga wa kienyeji ,ama matabibu
ambao huchukua jukumu la kuwatibu majambazi waliojeruhiwa hivyo alitoa
salamu kwao kuwa atakaebainika watamkamata na kumchukulia hatua kali za
kisheria .
"Polisi
ilipambana na majambazi watano ,kwa dhumuni la kupora fedha nyumbani kwa
mama huyo mhasibu wa vicoba ambae alitoa fedha kwa ajili ya kugawia
wanachama wenzie" alisema .
Kamanda
Shanna alieleza kwamba ,katika mapambano hayo kikosi cha polisi
kilishambulia majambazi wanne na mmoja alikimbia akiwa amejeruhiwa
vibaya.
Alisema mbali ya
hayo, walipopekua gari walikuta na kukamata silaha mbalimbali ikiwemo
silaha ya kisasa ya kivita AK 67 inayotumia risasi 30 kwa wakati
mmoja,magazine mbili , bunduki mbili na risasi 54 .
Pia
walikamata pistol mbili bandia ,toy la umbile la kiume,na plate namba
mbili zenye namba za usajali halisi , redio call plasta ngumu ya kuziba
mdomo,kofia nyeusi ya kuficha macho na pingu .
Kamanda huyo alisema majambazi yasijaribu kufanya uhalifu kwani wapo vizuri kupambana na wahalifu .
Nae
mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama Mkoani Pwani, mkuu wa Mkoa
huo Evarist Ndikilo alisema Mkoa bado upo shwari kwani wapo vizuri
kudhibiti uhalifu wowote utakaojitokeza.
Alimpongeza kamanda Shanna pamoja na askari polisi ambapo hakuna askari aliyepoteza Maisha.
"Kauli
mbiu yetu ya mkoa ni Utaingia kwa hiari yako lakini hautotoka salama
,kwakuwa Mkoa huu ni wa Viwanda na uwekezazji tunahitaji amani na
utulivu.
Ndikilo aliwahakikishia wawekezaji Mkoa wa Pwani upo salama na jeshi la polisi lipo tayari kulinda wananchi na mali zao .
Alisema wale ambao wana nia mbaya ya kukimbiza wenye nia ya kuwekeza wajue hawatafanikiwa .
Ndikilo alifafanua hakuna nafasi ya kufanya mambo ya ajabu ajabu na atakaethubutu atapata malipo anayoyahitaji.
Mganga
mfawidhi wa hospital ya wilayani ya Kisarawe ,dokta Yona Kabata alikiri
kupokea miili ya marehemu ya watu wanne kutoka kwa maafisa wa
polisi,majira ya saa 4 :40 asubuhi April 20.



0 Comments