Waziri wa Dkt. Medard Kalemani (mwenye shati nyeusi) akitoa
maelekezo Aprili 17, 2018 wilayani Urambo baada ya kukagua njia ya kupeleka umeme vijiji
unatekelezawa chini ya miradi inayosimamiwa na Wakala wa Umeme Vijiji awamu ya
Tatu.
Mbunge wa Jimbo la Urambo Magreth Sitta(kulia) akizungumza na wakazi wa kijiji cha Jioneemwenyewe Kata ya Songambele wakati wa sherehe za uwashaji wa umeme zilizozunduliwa na Waziri wa Nisha Dkt Medard Kalemani (hayupo katika picha) jana. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Urambo Angelina Kwingwa.
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani(mwenye miwani) na Mbunge wa Urambo Magreth Sitta na viongozi wengine wakikata utepe wa uzinduzi wa uwashaji wa umeme wa REA katika Kijiji cha Jionee Mwenyewe kata ya Songambele
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (mwenye miwani) akiwapungua mkono wananchi wa Kijiji cha Jionee Mwenyewe kata ya Songambele wakati wa sherehe za uwashaji umeme wa REA
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akibonyesha kitufe kuwasha umeme katika Kijiji cha Jionee Mwenyewe Kata ya Songambele baada ya kukamilika kwa mradi wa uwekaji wa miundombinu katika eneo hilo.
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (mwenye miwani) na Mbunge wa Urambo Magreth Sitta(kushoto) na wananchi wa kiijiji cha Jionee Mwenyewe kata ya Songambele wakishangilia mara baada ya uzinduzi wa uwashaji wa umeme katika eneo hilo.
Baadhi ya wanakijiji wa Jionee Mwenyewe Kata ya Songambele wakisikiliza Hotuba ya Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (hayupo katika picha ) mara baada ya kuzindua uwashaji wa umeme katika Kijiji chao

Waziri
wa Nishati Medard Kalemani akimpongeza Diwani wa Kata ya Vumilia kupitia ACT
Wazalendo Kassim Shushu (kushoto) baada ya kumkabidhi eneo la shamba lake
linalokadiriwa kuwa ekari moja kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Kupozea umeme.
Picha na Tiganya
Vincent
NA TIGANYA VINCENT-RS
TABORA
SERIKALI imesema
ni marufuku kwa Wakandarasi na Wataalamu kuruka nyumba wakati wa uunganishaji
wa umeme kwa wananchi kupitia Mradi kabambe
wa kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya
Tatuunatekelezwa na Wakala wa Umeme Vijijini (REA).
Kauli hiyo
ilitolewa Aprili 17, 2018 wilayani Urambo na Kaliua na Waziri
wa Dkt. Medard Kalemani wakati alipokuwa akigaua utekelezaji wa
zoezi la usambazaji wa umeme wa REA katika maeneo hayo.
Alisema ni
marufuku kuruka nyumba hata kama ni nyasi kama mwananchi anataka umeme na
amelipa shilingi 27,000 za kuunganishiwa umeme.
Kalemani alisema
kuwa mpango wa Serikali ni kuhakikisha umeme unafika katika vijiji na vitongoji
vyote na kwa wananchi wote bila kubagua.
“Nawaagiza
Wakandarasi na Wataalamu wote hakuna kuruka nyumba wala kubagua nyumba kwa
sababu ya kuwa imeezekwa kwa nyasi…umeme ni nyumba kwa nyuma , kaya kwa kaya..,
hata kama mtu hajakamisha nyumba yake kama kuna mti karibu na nyumba yake
wekeeni hata hapo ili iwe rahisi kuingiza umeme atakapokuwa amekamisha nyumba
yake” alisisitiza Waziri huyo.
Alisisitiza kuna
mtindo wa Wakandarasi kuchagua nyumba wakati wanapotekekeza majukumu yao ya
kuwaweka umeme , na kusema kuwa kwa hivi sasa hilo ni marufku umeme ni kwa wote
wanaotaka.
Waziri huyo wa
Nishati aliongeza kuwa ni marufuku kuwatoza wananchi wanaotaka kuunganishiwa
umeme zaidi ya shilingi 27,000/- na kutoa wito kwa mwananchi atayetozwa zaidi
ya kiasi hicho atoe taarifa ili hatua kali dhidi ya wahusika ziweze kuchukiwa.
Aidha alitoa wito
kwa wananchi kuchangamkia fursa hiyo ya kuunganishiwa kwa gharama hizo kwani
baada ya hapo itabidi walipie kulingana na taratibu za Shirilka la Ugavi wa
umeme Tanzania(TANESCO)
Katika
hatua nyingine Waziri huyo wa Nishati amemupongeza Diwani wa Kata ya
Vumilia Wilayani Urambo Kassim Shushu kwa kutoa eneo lake kwa ajili ya
kuwapatia TANESCO ili wajenge kituo cha kupozea umeme.
Alisema kitendo
hicho cha Diwani wa Kata ya Vumilia kupitia ACT Wazalendo ni cha kizalendo na
kimeonyesha kuwa maendeleo hayana chama na baada ya kukamilisha mradi TANESCO
itabidi waone jinsi ya kumpa mkono wa shukurani.
Dkt . Kalemani
alisema baada ya Shirika lake la la Ugavi wa Umeme Tanzania(TANESCO)
litajenga Kituo kidogo cha kupozea umeme (sub station) katika Kijiji hicho cha Uhuru
ili kuboresha upatikanaji wa huduma ya umeme kwa wananchi wa Wilaya ya
Kaliua na Urambo na maeneo jirani.
Alisema Kituo
kikingine kitajengwa mpakani mwa Tabora na Kigoma kwa ajili ya kuuwezesha na
Mkoa wa Kigoma kuwa na umeme wa uhakika.
Waziri huyo wa
Nishati alisema hatua hiyo itasaidia kupunguza tatizo la kukatika kwa umeme
katika maeneo hayo.

0 Comments