Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame
Mbarawa akisisitiza jambo wakati akifungua Mkutano wa Nane wa Wiki ya Kijani wa
Shirika la Mawasiliano Duniani (ITU) unaohusu namna ya kutumia TEHAMA kuendana na
mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika Zanzibar
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame
Mbarawa (kulia) akizungumza na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Viwango wa Shirika la Mawasiliano Duniani (ITU) Dkt.
Chauseb Lee kuhusu ushirikiano baina ya Tanzania na ITU kuhusu namna ya kutumia
TEHAMA kuendana na mabadiliko ya tabia nchi wakati wa Mkutano wa Nane wa Wiki
ya Kijani uliofanyika Zanzibar
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
Mhandisi James Kilaba (katikati) akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano wakati wa mkutano wa Nane wa Wiki ya Kijani wa Shirika
la Mawasiliano Duniani (ITU) uliofanyika
Zanzibar kuhusu namna ya kutumia TEHAMA kuendana na mabadiliko ya tabia nchi.
Kushoto ni Katibu Mkuu wa Mawasiliano wa Wizara hiyo, Dkt. Eng. Maria Sasabo
Mkurugenzi wa Shirika la Mawasiliano Duniani (ITU) wa
Mawasiliano na Viwango Dkt. Chauseb Lee akifafanua jambo kwa wadau wa TEHAMA
wakati wa mkutano wa Nane wa Kijani kuhusu namna ya kutumia TEHAMA kuendana na
mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika Zanzibar
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame
Mbarawa (aliyeketi katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa TEHAMA
kwenye mkutano wa Nane wa Wiki ya Kijani wa Shirika la Mawasiliano Duniani
(ITU) unaohusu namna ya kutumia TEHAMA kuedana na mabadiliko ya tabia nchi
uliofanyika Zanzibar
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Sira Ubwa Mwamboya akisalimiana na Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Mhandisi James Kilaba wakati wa Mkutano
wa Nane wa Wiki ya Kijani wa Shirika la Mawasiliano Duniani (ITU) kuhusu namna
ya kutumia TEHAMA kuendana na mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika Zanzibar.
Katikati ni Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Mhandisi
Peter Ulanga
Wadau wa Shirika la Mawasiliano Duniani (ITU) wanaohusika
na masuala ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) wamekutana Tanzania
kutoka nchi mbali mbali duniani kwenye Mkutano wa Nane wa Wiki ya Kijani kwa
lengo la kujadiliana namna ya kutumia TEHAMA kuendana na mabadiliko ya tabia nchi
yanaoendelea kutokea duniani.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Prof. Makame Mbarawa amefungua mkutano huo uliofanyika
Zanzibar ambao umeandaliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) na Mamlaka
ya Mawasiiano Tanzania (TCRA) wakiwa waandaji na wenyeji wa mkutano huo.
Wakati akifungua mkutano huo, Prof. Mbarawa amewataka
wataalamu wote wa TEHAMA kutoka sehemu mbali mbali duniani kutumia mkutano huo
kujadiliana, kuweka mikakati na miongozo
ya namna ya kutumia huduma na bidhaa za TEHAMA kwa maendeleo ya uchumi na
viwanda ikiwa ni pamoja na mbinu za kutabiri na kudhibiti majanga yanayotokea
kuendana na mabadiliko ya tabia nchi kwa kutumia TEHAMA.
Amewataka washiriki wa mkutano huo kubadilishana uzoefu
na kujadiliana namna ya kutumia TEHAMA kulinda mazingira, kufungua fursa za
kiuchumi, kuwa na miji ya kisasa ambayo inaendeshwa na kusimamiwa kwa kutumia
TEHAMA illi kuhakikisha kuwa TEHAMA inatumika kutunza mazingira ili kupunguza
uchafuzi wa mazingira kutokana na mabaki ya vifaa na huduma za TEHAMA na kuweza
kurudufu mabaki hayo ii kulinda usalama wa mazingira na yaweze kutumika kwa
matumizi mengine.
Amefafanua kuwa Tanzania imejenga Mkongo wa Taifa wa
Mawasiliano wenye urefu wa zaidi ya kilomita 25,000 ambao umeunganishwa kwenye
taasisi za Serikali na sekta binafsi na kwenye nchi za jirani ambazo
hazijapakana na bahari ambapo umewezeshaji utoaji wa huduma za mawasiliano
nchini ambapo hadi hivi sasa tuna jumla ya watanzania milioni 45 wanaotumia
simu za mkononi, milioni 23 wanaopata huduma ya intaneti na milioni 20
wanaotumia huduma za kielektoniki kama vile kutuma na kupokea pesa, “watu hao
wote wanatumia vifaa mbalimbali vya kielektroniki, baada ya muda vifaa hivi
vitakuwa havifanyi kazi, vimepitwa na wakati, sasa inatakiwa tuvitoe kwenye
soko vizuri bila kuharibu mazingira ambayo tunayatumia, sasa tukikaa hapa na
wataalamu hawa tunaamini tutajifunza njia mbali mbali ambazo zinatumika duniani
katika kuharibu hivi vifaa vya kielektroniki ambavyo vimeshapitwa muda wake”
amesema Prof. Mbarawa.
Naye Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano na Viwango wa
Shirika la Mawasiliano Duniani (ITU) Dkt.
Chaesub Lee amewataka wataalamu hao kujadiliana na kupeana uzoefu wa kutoka
kwenye nchi zao za kutumia fursa za TEHAMA kuongeza mzunguko wa uchumi na
viwanda duniani, kutumia bidhaa na huduma za TEHAMA kuhifadhi na kulinda
mazingira na kuchakata bidhaa na huduma za mawasiliano ambazo zimepitwa na muda
wake au kuharibika ambapo ITU iko tayari kushirikiana na nchi husika katika
nyanja ya utalaamu, ushauri na utekelezaji wa mipango na mikakati mbalimbali ya
namna ya kutumia TEHAMA kuendana na mabadiliko ya tabia nchi kulingana na mahitaji
ya nchi husika.
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Sira Ubwa Mwamboya wakati akifunga mkutano huo,
amewakaribisha washiriki hao kutembelea vivutio mbali mbali vya kiutalii
vilivyopo kwenye visiwa hivyo.
Mkutano huo umeandaliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote
kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kwa niaba ya Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Imeandaliwa
na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara
ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
0 Comments