Mbunge wa Mafinga Mjini, Cosato
Chumi ameitaka Serikali kuhakikisha inasambaza mbolea kwa bei nafuu na kwa
wakati.
Chumi amesema hayo wakati akichangia
Hotuba ya Waziri Mkuu Bungeni.
'Mhe Mwenyekiti, serikali imekiri
kuwa usambazaji wa mbolea ulikuwa 64% mana yake ni kuwa 36% ya wakulima
hawakupata mbolea'
'Sio hivyo tu, hata hiyo 64%
hawakupata mbolea kwa wakati, sio haki kabisa, mkulima wa Itimbo, Kitelewasi,
Isalavanu apelekewe mbolea ya kupandia mwezi February wakati uandalizi wa
mashamba unaanza mapema Oktoba.'
Kuzuia kuuza ziada ya mazao ni
kuwaonea wakulima
Akizungumzia wakulima kuuza mazao
yao,nje ya nchi, Chumi alisema kuna ziada ya tani 2.6milioni ya chakula, lakini
Hifadhi ya Taifa ya Chakula imenunua tani 26,000(elfu ishirini na sita tu), afu
mkulima anazuiwa kuuza mahindi yake, jambo ambalo sio sawa.
Tunawafanya wakulima wa nchi hii
kama raia daraja la pili (second citizens),
mbolea tuwacheleweshee, ziada ya
mazao yao tuwafungie kuuza, hii sio sawa' alisisitiza Mbunge huyo na kuongeza
kuwa ni vizuri serikali ikaangalia changamoto ilizokutana nazo katika
usambazaji wa mbolea mwaka huu na kuboresha mazingira ili kumsaidia mkulima
kupata mbolea kwa bei nafuu, kwa wakati na pia kuuza ziada ya mazao.
Awataka Wawekezaji Mafinga kuwajali
wafanyakazi
Akizungumzia haki za wafanyakazi,
Chumi alisema kuwa anapongeza jitihada za Rais John Magufuli kuvutia
wawekezaji, lakini akaitaka Wizara ya Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi na Ajira
kutupia jicho haki za wafanyakazi kwenye Viwanda vya Mafinga.
Uchumi wa Viwanda lazima uendane na
welfare ya wafanyakazi, itakuwa haina mana kuwa na viwanda lakini hali za
wafanyakazi zinakuwa duni, lazima walipwe vizuri, waangaliwe huduma za afya na
kulipiwa nssf , alisisitiza Mbunge huyo.
Akifafanua, alisema sio haki
mfanyakazi anatoka Changarawe, anatembea mpaka kilometa nne kwenda kazini, sio
haki.
ni hatari sana, unakuta mama anaamka
saa kumi alfajiri kuwai kazini ambako nako halipwi vizuri, nikuombe mama
Jenista Mhagama (Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu) na kaka yangu Mavunde
(Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Vijana) nadhani ni
mdogo wangu kufika Mafinga na kutoa maelekezo.
Apongeza Mhe Rais kukutana na
Wafanyabiashara, ashauri akutane nao Kisekta
Tumeona ambavyo Jumuiya ya
wafanyabiashara walieleza kero zao na Mhe. Rais na Rais akaagiza Mawaziri
wazifanyie kazi, lakini nimuombe Mhe Rais akutane na Wafanyabiashara kisekta
mana siku ile wote tuliona muda ulikuwa mdogo kwa mfano anaweza kukutana na
sekta ya usafirishaji.
Akizungumza baadae na Mwandishi
wetu, Chumi alisema kuwa mazingira wanayofanyia kazi wafanyakazi kwenye Viwanda
vya Mafinga hayaridhishi na wanapolalamika kwa baadhi ya viongozi taarifa
hurejeshwa kwa wenye viwanda kwa siri na matokeo yake mlalamikaji hutafutiwa
visa na kufukuzwa kazi.

0 Comments