Mkuu
wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (mwenye
kofia ya kijani) na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa na ile ya Wilaya ya Igunga
wakiliangalia Basi la City Boy lilopata ajali ya kugonagana uso kwa uso na lori
siku ya Jumatano usiku Aprili 4, 2018.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akiliangalia Basi la City Boy lilopata ajali ya kugonagana uso kwa uso na lori siku ya Jumatano usiku mara baada kuongozana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na ile ya Wilaya ya Igunga kutembelea eneo la tukio.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (aliye na kofia ya kijani) akiwa kwenye ilipotokea ajali ya Basi la City Boy kugonagana uso kwa uso na lori siku ya Jumatano usiku.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akiwafariji majeruhi wa ajali ya Basi la City Boy iliyogongana uso kwa uso na lori siku ya Jumatano usiku mara baada kutoka katika ilipotokea ajali wilayani Igunga
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(wa pili kushoto) akifafanua jambo jana wakati wa kikao cha kujitathimini kwa ajili ya kuja na majibu ya kuondoa ajali za barabarani mkoani humo kichofanyika jana Wilayani Igunga na kuhudhuriwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Tabora na ile ya Wilaya ya Igunga na wadau mbalimbali wa usafiri. Wengine ni Mkuu wa Wilaya ya Igunga John Mwaipopo(wa pili kulia) Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Wilbroad Mtafungwa(kushoto) na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Hajjat Rukia Manduta.

NA TIGANYA VINCENT
RS TABORA
KAMATI ya Ulinzi na
Usalama ya Mkoa wa Tabora na Wadau wa Usafiri wamependekeza uanzishwaji wa
matumizi ya vitabu(log book) kwa magari ya mizigo ili kudhibiti madereva
kusafiri mwendo mrefu bila kupumzika na hivyo kusababisha ajali kwa magari yao au kugongana uso kwa uso na
magari mengine kutokana na uchovu.
Tamko hilo limetolewa
jana wilayani Igunga na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri mara baada ya
kikao cha kujitathimini kwa ajili ya kuja na majibu ya kuondoa ajali za
barabarani mkoani humo.
Mkuu huyo wa Mkoa
alisema vitabu hivyo vitasaidia kuonyesha muda alitoka , mahali alitoka na kama
amesafiri muda mrefu atalazimisha apumzike ili kuepusha ajali.
Alisema malori yamekuwa
yakisafiri mwendo mrefu bila hata dereva wake kupumzika jambo ambalo
limesababisha magari hayo yapate ajali au wakati mwingine yawe chanzo
kinachosabisha ajali katika magari ya abiria.
Mwanri
alisema kwa kulitambua hilo wanaona wakati umefika kwa magari ya mizigo
nayo kuwa na vitabu(log book ) inayoonyesha muda alianza safari katika
kituo chake cha kwanza na muda alipo baada ya kusimamishwa ili kuona
kama kweli amezingatia matawaka ya kitaalamu na sharia ya kutokwenda
kasi.
Alisema kitaalamu dereva
anatakiwa aendeshe chombo cha moto kwa muda usiozidi saa nane lakini mara
nyingi madreva wa malori wamekuwa wakiendesha magari yao hata zaidi ya muda
huo jambo ambalo limekuwa kiwasababisha baadhi yao kuendesha huko wakisinzia na kupelelea gari kukosa mwelekeo.
Mwanri
alisema ili kuepukana na hilo wadau wamependekeza wammiliki wa gari wa
ya mizigo ya masafa marefu ni vema wawe na madereva wawili ili
wasaidiane.
Mkuu huyo wa Mkoa
alisema hatua nyingine ambayo wameamua kuichukua ni pamoja na kuongeza askari na
magari ya doria katika barabara kuu ya Igunga, Nzega kwenda Mwanza na Shinyanga.
Alisema hatua hii
inalenga kupambana na madreva ambao nyakati za usiku wakwenda mwendo mkali kwa sababu
ya kujua kuwa nyakati hizo tochi hazifanyi kazi.
Mwanri aliongeza kuwa Wadau
wa usafiri wameiagiza Wakala wa Barabara Tanzania(TANROADS) mkoani Tabora kuhakikisha
wanaziba mashimo yaliypo katika barabara kuu zote ili kuondoa uwezekano wa
yenyewe kuwa chanzo cha ajali za barabarani.
Aidha alisema kuwa
Wadau wamekuwabaliana kuwa ukaguzi wa madereva na magari katika barabara kuu
zinazopita Mkoani Tabora utakuwa unafanyika kila siku ili kujihakikishia kama gari linazo
breki, taa zifanya kazi vizuri , matari yako vizuri na dreva ajatumia kilevi.
Alisema hatua hiyo
inalenga kujihakikishia kama chombo cha usafiri na dreva wake yuko katika hali
nzuri.
Hivi karibuni (4
/4/2018) kulitokea ajali ambapo basi la abiria Kampuni ya City Boy yenye namba
T 983 DCE iligongana uso kwa uso lori lenye namba T .486 ARB Mitsubishi Fuso wilayani
Igunga na kusababisha watu 12 kufa palepale na mmoja kufia katika Hospitali ya
Rufaa Bugango.
Taarifa za awali
zinaoonyesha kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva wa Fuso uliosababisha
tairi kupasuka na gari kuhamia upande wa basi.
Lori hiyo lilikuwa na
viazi ambavyo lilivitoa Njombe Mwisho

0 Comments