Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro akifafanua jambo kuhusu Watumishi wa Umma 4,812 watakaonufaika na fursa 659 za mafunzo ya muda mfupi na mrefu zilizotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kwa mwaka 2018.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro akizungumza na Waandishi wa Habari leo Ukumbi wa Idara ya Habari - Bunge kuhusu Watumishi wa Umma 4,812 kunufaika na fursa 659 za mafunzo ya muda mfupi na mrefu zilizotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kwa mwaka 2018.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro akizungumza na Waandishi wa Habari leo Ukumbi wa Idara ya Habari - Bunge kuhusu Watumishi wa Umma 4,812 kunufaika na fursa 659 za mafunzo ya muda mfupi na mrefu zilizotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kwa mwaka 2018.
Watumishi wa Umma
4,812 kunufaika na fursa 659 za mafunzo ya muda mfupi na mrefu zilizotolewa na
Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kwa mwaka 2018.
Katibu Mkuu, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro amesema hayo leo wakati
wa kikao na Waandishi wa Habari kilichofanya ukumbi wa Idara ya Habari-Bunge
mjini Dodoma.
Dkt. Ndumbaro ameainisha
kuwa, mafunzo hayo yamelenga katika eneo la Uhandisi wa Viwanda, Mawasiliano na
Usafirishaji, Kilimo, Elimu, Afya, Biashara na Uchumi, TEHAMA na Utawala Bora
ambayo ndio maeneo ya kipaumbele katika Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa miaka
mitano (2016/17 hadi 2020/21).
Dkt. Ndumbaro ametoa
wito kwa Watumishi wa Umma kuchangamkia fursa hizo ambazo zitawajengea uwezo wa
kiutendaji katika kutoa huduma kwa umma.
Dkt. Ndumbaro ametoa
wito kwa waajiri kuwawezesha watumishi walio chini yao kuhudhuria mafunzo hayo
kwa mujibu wa Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo ya Utumishi wa Umma iliyopo
kwa kuzingatia mipango ya mafunzo.
Akitoa shukrani kwa
niaba ya Serikali, Dkt. Ndumbaro ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Watu wa
China kwa kutoa fursa hizo. Aidha, amewashukuru na wadau wengine wa maendeleo
ambao ni India, Australia, Japani, Jamhuri ya Korea, Singapore, Misri na
Uholanzi kwa kushirikiana na Serikali kuwajengea uwezo wa kiutendaji Watumishi wa
Umma nchini kwa kutoa fursa za mafunzo 1,865 kati ya mwaka 2015/16 na 2017/18.
Fursa hizo
zinapatikana kupitia tovuti ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora (www.utumishi.go.tz).
IMETOLEWA
NA:
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
OFISI YA RAIS (UTUMISHI)
TAREHE 17
APRILI, 2018
0 Comments