Na Mwamvua Mwinyi,Bagamoyo
Halmashauri
ya Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani inafanya tathmini ya mafuriko ya
mvua yaliyotokea ili waweze kununua dawa kwa ajili ya kuua wadudu
wanaoweza kuleta magonjwa mbalimbali yatokanayo na kutuama kwa maji ya
mvua.
Hayo yalisemwa Bagamoyo na mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Fatuma Latu wakati wa kikao cha baraza la madiwani.
Latu
alisema kutokana na tatizo la maji kutuama katika maeneo mengi yakiwemo
kwenye makazi ya watu,inabidi kuwekwa dawa ya kuua wadudu hao .
Aidha
alieleza athari za mvua ni kubwa , kila kata kupitia madiwani
wamekubaliana na madiwani ,kamati husika zitakaa ili kufuatilia suala
hilo.
Latu alisema kuwa suala hilo lililetwa kwenye baraza kama dharura kutokana na hali ya mvua zinazoendelea kunyesha hapa nchini.
Awali
Diwani wa kata ya Makurunge Paul Kabile alisema kuwa mvua hizo zimeleta
athari kubwa sana kwa wananchi ambapo wamezungukwa na maji ambayo
yanaweza kuleta athari ya magonjwa ya mlipuko.
Kabile
alisema ,athari ni kubwa ambapo baadhi ni uharibifu wa
makazi,barabara,miundombinu mbalimbali hali inayofanya wananchi wawe na
wakati mgumu kuingia au kutokana kwenye majumba yao.
Naye
Diwani wa viti maalum Shumina Abdala alisema kuwa licha ya makazi
kuathiriwa na mvua hizo hata taasisi za umma kama shule,zahanati na
vituo vya afya.
Abdala
alisema kuwa kuna haja ya kuwa na dharura juu ya suala la kupatikana
dawa za kuwa wadudu wanaoweza kuleta magonjwa kwani uchafu umetapakaa
kila mahali.
Mkurugenzi halmashauri ya Bagamoyo,Mkoani Pwani Fatuma Latu akizungumza katika baraza la madiwani.
(Picha na Mwamvua Mwinyi)
Diwani wa viti maalum ,Shumina Abdala
(mwenye aliyeaimama mwenye blauzi nyekundu)akizungumza jambo wakati wa
baraza la madiwani wilayani Bagamoyo.
(Picha na Mwamvua Mwinyi)
Baadhi ya madiwani wa wilaya
ya Bagamoyo, wakifuatilia kwa makini yaliyojiri katika baraza la
madiwani wilayani hapo .
(Picha na Mwamvua Mwinyi)



0 Comments