·
Yatangaza Ofa Kabambe
·
Watangazaji Nguli Kurindima kwa Kiswahili
·
Wateja kutazama popote walipo
·
Mtanange huo kuonyeshwa live kwenye vifurushi
vyote
·
Channel maalum 6 kuonyesha Michuano hiyo
katika HD
Huku zikiwa zimebaki siku chache kwa
kinyang’anyiro cha Kombe la Dunia 2018 kuanza nchini Urusi, Kampuni ya
MultiChoice Tanzania imetangaza neema kwa Watanzania kwa kutoa ofa maalum kwa
wateja wapya, huku ikitenga chaneli 6 maalum zitakazoonyesha michuano hiyo
katika kiwango cha HD Kiswahili katika vifurushi vyote vya DStv. pamoja na
kuwawezesha wateja wake wote kufuatilia michuano hiyo kwa Lugha ya “Hii ni zaidi ya ofa”
Anasema Ronald Shelukindo, Mkuu wa Uendeshaji
wa MultiChoice Tanzania wakati akitangaza ofa hiyo jijini Dar es Salaam jana.
“Sasa tunataka watanzania waweze kupata burudani ya kombe la dunia 2018 kwa
namna tofauti kabisa. Kwanza kwa pamoja na kifurushi cha miezi miwili bure!”
alisema Shelukindo na kuongeza wateja wapya wataweza kujiunga kw shilingi
79,000 tu na kupata seti ya DStv moja kwa moja kwa lugha ya Kiswahili ambapo
tuna timu ya watangazaji mahiri wa “Kama hiyo haitoshi, wateja wote wa DStv,
sasa wataweza kupokea matangazo ya soka hapa nchini watakaowaletea watanzania
burudani hii”
Amesema mbali na ofa hiyo na kutangazwa kwa
michuano hiyo kwa lugha ya Kiswahili, pia DStv imetenga chaneli 6 mahususi
kabisa kwa ajili ya michuano hiyo pamoja na kuhakikisha kuwa wateja wanaweza
kutazama DStv popote walipo wakati wowote kwa kutumia vifaa kutumia hadi vifaa
vitano tofauti ambavyo vyote huunganishwa na dikoda yako kama simu, laptop na
tablet. “Hivi sasa ukipakua app yetu ya DStv Now, unaweza hivyo kuwawezesha wanafamilia kutazama vipindi tofauti
kwa wakati mmoja” alisema Shelukindo.
Akitoa maelezo kuhusu jinsi DStv
ilivyojizatiti kuwahakikishia watanzania burudani isiyo na kifani msimu huu wa
kombe la dunia, Mkuu wa Masoko wa MultiChoice Tanzania Alpha Mria, amebainisha
kuwa DStv itaonyesha michuano hiyo katika vifurushi vyake vyote, angavu yanni
HD. hivyo wateja wote wa DStv watafurahia michuano hiyo tena katika muonekano “Kwakeli
msimu huu wa kombe la Dunia, kila atakayekuwa na DStv atakuwa anapata hasa kile
anachostahili kwani mechi zote zitaonekana live, kwenye HD na kwenye vifurushi vyote,
huku pia zikitangazwa kwa lugha mbalimbali ikiwemo lugha ya Kiswahili” alisema
Alpha
Amesema kwa wale wanaotaka kufuatilia kwa Kiingereza wataweza
kuona kupitia DStv, wale wa Kireno wataona kupitia DStv, wale wa Kifaransa pia
wataona kupitia DStv, na kikubwa zaid sisi watanzania tutaweza kufuatilia kwa
lugha yetu adhimu ya Kiswahili kupitia DStv.
“Tumejipanga, kuwapa watanzania burudani ya aina yake msimu huu wa
kombe la Dunia” Alisisitiza Alpha.
Katika uzinduzi huo, DStv iliwatambulisha rasmi watangazaji wa
soka ambao watakuwa wakiwaletea watanzania matangazo hayo kwa Kiswahili ambapo
majina makubwa ya watangazaji na wachambuzi Kibonde, Edo Kumwembe, Ibrahim
Masoud - Maestro na Oscar Oscar. wa soka yamo. Waliotambulishwa ni Aboubakary
Liongo, Maulid Kitenge, Ephaim
Wakiongea baada ya kutambulishwa, watangazaji na wachambuzi hao mahiri wa soka
wamesema wamejizatiti kikamilifu kuhakikisha kuwa wanawaletea matangazo na
uchambuzi wa kina ili kuhakikisha kuwa kila mpenda soka anafurahia na kuyaelewa
vizuri mashindano hayo.
hao.
Pia
wachezaji kadhaa wa klabu za Simba na Yanga walihudhuria hafla hiyo iliyokuwa
ya kufana sana.
0 Comments