Mrasimu ramani Mwandamizi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw.
Benedict Mgambi akieleza kwa waandishi wa habari faida za kutumia mfumo wa ukusanyaji na
usambazaji wa taarifa za kijiografia
wakati wa ziara yao iliyonga kujionea jinsi Ofisi ya hiyo inavyotekeleza
majukumu yake katika ukusanyaji wa taarifa mbalimbali ikiwemo sense na tafiti
zinazofanywa kwa kutumia mfumo huo wa kisasa.
Mtaalamu
wa masuala ya Jiografia kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Matha Macha akitoa maelezo kuhusu namna mfumo huo
unavyofanya kazi.
Mrasimu
ramani msaidizi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Rahim Mussa
akisisitiza kuhusu namna mfumo huo unavyochochea maendeleo.
Mrasimu ramani Mwandamizi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw.
Benedict Mgambi akiongoza ujumbe kutoka
Ofisi ya Taifa ya Takwimu kutembelea
kijiji cha Sasa Wilaya ya
Chamwino ambapo ujumbe huo umeambatana
na waandishi wa habari kujionea mfumo wa ukusanyaji na usambazaji wa taarifa za
kijiografia wakati wa ziara yao iliyonga
kujionea jinsi Ofisi ya hiyo inavyotekeleza majukumu yake katika ukusanyaji wa
taarifa mbalimbali ikiwemo sense na tafiti zinazofanywa kwa kutumia mfumo huo
wa kisasa.
Mwenyekiti wa
kijiji cha Sasa Wilaya ya
Chamwino ambapo ni ujumbe wa NBS na
waandishi wa habari walitembelea
kujionea jinsi mfumo wa
ukusanyaji na usambazaji wa taarifa za kijiografia wakati wa ziara yao iliyonga kujionea jinsi
Ofisi ya hiyo inavyotekeleza majukumu yake katika ukusanyaji wa taarifa
mbalimbali ikiwemo sense na tafiti zinazofanywa kwa kutumia mfumo huo wa
kisasa.
(Picha
zote na Frank Mvungi- MAELEZO)
.............................................................
Na Beatrice Lyimo-
MAELEZO, Dodoma
Ofisi ya Taifa ya
Takwimu (NBS) imeanzisha mfumo wa ukusanyaji wa taarifa kwa kutumia teknolojia
mpya na ya kisasa ya kielektroniki kwa njia ya satelaiti na Vishikwambi.
Akizungumza na waandishi
wa habari leo mkoani Dodoma mrasimu ramani mwandamizi na msimamizi wa Sehemu ya
mfumo wa Ukusanyaji na Usambazaji wa taarifa za Kijiografia (GIS) Benedict
Mgambi amesema kuwa lengo la mfumo huo ni kuboresha ukusanyaji wa taarifa na tafiti mbalimbali kwa
ajili ya maendeleo ya nchi.
Mgambi amesema kuwa
teknolojia hii mpya imerahisisha kwa kiasi kikubwa ufanyaji kazi ikilinganishwa
na taratibu zilizokuwa zikitumika awali.
“Awali tulikuwa tunatumia
teknolojia ya duni ambapo mchakato wake ulihusisha watu wengi, gharama kubwa
ila kwa sasa hivi kila kitu kinafanyika eneo husika la tafiti na kutumwa moja
kwa moja makao makuu” amesema Mgambi
Aidha Mgambi amesema
kuwa zoezi hilo limeshirikisha wadau mbalimbali ikiwemo, TAMISEMI, Wizara ya
Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ,Wizara ya Maliasili na utalii pamoja na TAMISEMI.
Kwa upande wake Mtaalamu
wa Masuala ya Kijiografia (NBS) Martha Macha amesema kuwa mfumo huo
umerahisisha utendaji kazi wao kwani unasaidia kutambua mipaka mbalimbali kati
ya kitongoji kimoja na kingine.
“Vifaa hivi vinafanya
kazi kubwa kwa muda mfupi na pia vinafanya kazi kwa ubora ule unaohitajika kwa
kuona vielelezo mbalimbali vitakavyokuwezesha kufanya kazi kwa urahisi”
amefafanu Bi. Macha.
Mpaka sasa vijii
vitano vya Sasajila, Suli, Fufu, Champumba na Chiboli Wilaya ya Chamwino Mkoa
wa Dodoma vimefanyiwa majaribio ya mfumo huo.

0 Comments