Waziri
wa Madini Mhe. Angellah Kairuki
akiwasilisha hotuba ya makadirio ya
mapato na matumizi ya Fedha ya Wizara hiyo kwa mwaka 2018/2019 leo Bungeni Jijini Dodoma.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Uratibu
Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akitoa maelezo Bungeni
kuhusu hatua zitakazochukuliwa na Serikali katika kuwalinda watoto wa
kike ambapo ameahidi kuwa Serikali itatoa taarifa rasmi kuhusu kuwepo kwa
baadhi ya watu wanaowadhalilisha kijinsia watoto wa kike na hatua zilizochukuliwa na Serikali.
Waziri
wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisisitiza
kuhusu mikakati ya Serikali kupambana na Janga la Ukimwi hapa nchini ikiwemo
kuhamasisha upimaji wa Virusi vya UKIMWI
hasa kwa wanaume kote nchini ili
wajue hali zao na kuchukua hatua stahiki.
Mkuu
wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Venance Mabeyo (wakwanza kushoto)
akifuatilia hotuba ya Waziri wa Madini Mhe Angellah Kairuki Bungeni Jijini Dodoma
leo.
Mwenyekiti
wa Tume ya Madini Prof. Idrissa Kikula aliyesimama (kushoto) na Mmoja wa
Makamishna wa Tume hiyo Prof. Abdulkarim Mruma wakitambulishwa Bungeni leo mara
baada ya kipindi cha maswali na majibu.
Sehemu
ya Viongozi wa Tume ya Madini na wageni
mbalimbali wakiwemo wakuu wa Mikoa yenye madini wakifuatilia hotuba ya
Waziri wa Madini Bungeni Jijini Dodoma leo.
Sehemu ya Wanafunzi waliofika Bungeni
kwa ziara ya mafunzo wakiwa ndani ya ukumbi wa Bunge wakati wa kipindi cha maswali
na majibu.
( Picha zote na Frank Mvungi- MAELEZO)
....................................................
Na: Lilian Lundo - MAELEZO,
Dodoma.
Serikali
imesema kuwa pamoja na huduma za bidhaa ya fedha kuamuliwa na nguvu ya
soko kwa upande wake imekuwa ikichua
hatua za kisera ili kuhakikisha kuwa riba za mikopo zinapungua katika soko hapa
nchini.
Hayo
yameelezwa leo Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.
Ashatu Kijaji alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Konde, Mhe. Khatibu Haji juu
ya Serikali inachukua hatua gani ili benki ziweze kupunguza viwango hivyo vya
riba?
"Baadhi
ya hatua zilizochukuliwa na Serikali kupitia Benki Kuu ni pamoja na kuzitaka
benki za biashara kutumia mfumo wa kuhifadhi na kutoa taarifa za wakopaji
(Credit Reference Bureau System). Aidha, Benki hiyo imekuwa ikitoa mikopo ya
muda mfupi kwa benki za biashara kwa kiwango cha asilimia 6.89," amesema
Dkt. Kijaji.
Dkt.
Kijaji amezitaja hatua nyingine zilizochukuliwa kuwa ni Benki Kuu kushusha riba
(Discount Rate) kutoka asilimia 16.0 hadi asilimia 9.0 pamoja na kupunguza
kiwango cha chini cha amana kinachotakiwa kuwekwa Benki Kuu na benki za
biashara (Statutory Minimum Reserve Requirememnt (SMR)) kutoka asilimia 10.0
hadi asilimia 8.0.
Vile
vile Serikali imeendelea kulipa malimbikizo ya madai yaliyohakikiwa kwa lengo
la kupunguza kiwango cha mikopo chechefu na kuchochea ukuaji wa shughuli za
kiuchumi.
Aidha,
amesema baada ya hatua hizo za kisera kuchukuliwa na Serikali, baadhi ya benki
za biashara hapa nchini zimeanza kupunguza riba za mikopo.
Ameongeza
kuwa, Serikali itaendelea kuchukua hatua za kisera ili kuhakikisha kuwa riba za
mikopo katika soko zinaendelea kupungua.

0 Comments