Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo ,alhaj Majid Mwanga ,akizungumza wakati wa
mkutano na wananchi,Kata ya Miono ,Bagamoyo ulioitishwa na Mkuu wa Mkoa
wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo.
Diwani wa Kata ya Miono Juma Mpwimbwi akizungumza wakati wa mkutano na
wananchi Kata ya Miono ,Bagamoyo ,ulioitishwa na Mkuu wa Mkoa wa
Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo.
Mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,akizungumza wakati wa
mkutano na wananchi Kata ya Miono,Bagamoyo. (Picha na Mwamvua Mwinyi)
Na Mwamvua Mwinyi, Miono
WAKAZI wa kata ya
Miono ,Bagamoyo Mkoani Pwani ,wamemtaka meneja wa Mradi wa Maji Safi
Chalinze (CHALIWASA) ,mhandisi Christer Mchomba, kusambaza maji bila
upendeleo kwani wanataabika kwa kipindi kirefu.
Aidha
wamemuangukia mkuu wa mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo kuingilia kati
tatizo hilo kwa kuangalia namna ya kupunguza kero ya maji inayowakabili
pamoja na maeneo mengine ya Bagamoyo na Chalinze.
Akizungumza
kwa niaba ya wakazi hao , wakati mkuu huyo wa mkoa alipokwenda
kuzungumza na wananchi katika kata hiyo ,Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo
,alhaj Majid Mwanga alisema CHALIWASA hali sio salama.
Alieleza
wanashangazwa kuona maeneo ambayo yanasambazwa maji na mawakala /watu
binafsi kwa niaba ya CHALIWASA kama kijiji cha Hondogo maji
hayakosekani kamwe.
Alhaj Mwanga alisema, hata msikitini maji yamekuwa mtihani kupatikana hali inayosababisha kero kwa watumiaji .
"Nikiwa
mwakilishi wako wilayani hapa ,nimeshashirikiana na viongozi wa
halmashauri, madiwani na Chama Cha Mapinduzi, Tumechukua hatua ya kwanza
kumtaka meneja CHALIWASA kuwapelekea taarifa kwanini maji hayasambazwi
kwa ratiba"
"Tumefanya kazi ya kutosha ,tumeweka ratiba
lakini bado ratiba sio rafiki kwa walaji wa maji si Miono ,Msata
,Kiwangwa ,Chalinze wala Lugoba "; alisisitiza alhaj Mwanga.
Alhaj
Mwanga alisema, kilio kikubwa kwa wakazi wa Chalinze ni maji suala
ambalo linarudisha nyuma juhudi za kimaendeleo kwa jamii.
Baadhi ya wakazi wa Miono akiwemo Rashid Hemed na Zakia Abdallah walisema, tatizo la maji ni kubwa katika kata hiyo.
Diwani
wa kata ya Miono Juma Mpwimbwi, alisema hali ya mradi mkubwa wa aina
hiyo iliyofikia ni mbaya na haileti taswira nzuri kwa jamii.
Alisikitika kutokuwa na maji ya uhakika kwa miaka mingi hali ambayo inakatisha tamaa wananchi.
"Mkuu
wa mkoa aingilie kati ama Rais dk.Joh Magufuli aje kujionea labda kauli
yake itasaidia kutatua changamoto ya mradi huu:;"Mradi huu sio rafiki
tena na jamii ;" alisisitiza Mpwimbwi.
Akizungumzia
kero hiyo ,Mkuu wa Mkoa wa Pwani ,mhandisi Ndikilo ,alisema bado kuna
shida ya maji na ni lazima kidogo kilichopo kigawanywe ili kila mmoja
anufaike.
Alisema inaonekana ratiba na mipango na utaratibu iliyowekwa kwa wananchi haiheshimiwi .
"Huu
ni mpango wa muda mfupi ,lakini hapa kuna ratiba ambayo haiheshimiwi
,kama ingekuwa inaheshimiwa basi Miono Kiwangwa wakazi wangekuwa
wanajipanga kuchota maji ili kuweka maji ya akiba"
Ndikilo
,alimtaka mhandisi wa CHALIWASA mhandisi Mchomba ,kukutana nae Jumanne
Mei 29 mwaka huu ofisini huku akiwa na majibu ya lengo lake la kutofuata
utaratibu uliowekwa kusambaza maji .
Hivi karibuni
mhandisi Mchomba ,alifafanua mradi huo una uwezo wa kuzalisha cubic
meters za maji 3,000 sawa sawa na lita 300,000 kwa siku .
Alisema
lita 15,000 huwa zikipotea njiani wakati wa kusambaza maji hali ambayo
wengi wao wanashangaa kuona kuna maeneo ambayo hayakosekani maji.
Mhandisi
Mchomba alibainisha ,awali mradi huo ulilenga vijiji 20 na wakazi
100,000 kwasasa vipo vijiji 86 huku wakazi wakifikia zaidi ya 200,000 .#
"Kwa
siku CHALIWASA tunazalisha lita laki tatu hadi tano kwa siku za maji,
yanayotolewa kwa mgao wa saa 6 kwa kila kijiji ndani ya Chalinze,
ikijumuisha na vingine vilivyopo maeneo ya Bagamoyo, Kibaha na Morogoro
vijijini," alisema Mchomba.




0 Comments