Mganga
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Dkt. Timothy Wonanji ,akisisitiza jambo wakati wa Mkutano wa mkutano wa “Cross-Border”
uliowakutanisha wataalamu wa Afya moja kutoka
katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro,
Manyara na Dodoma kujadili mikakati ya
kudhibiti ugonjwa wa Kimeta, Jijini, Arusha.
Mkurugenzi Msaidizi, Kitengo cha Epidemiolojia na Udhibiti wa Magonjwa, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Janneth Mghamba,akisisitiza jambo wakati wa Mkutano wa mkutano wa “Cross-Border” uliowakutanisha wataalamu wa Afya moja kutoka katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Dodoma kujadili mikakati ya kudhibiti ugonjwa wa Kimeta , Jijini, Arusha.
Baadhi ya Wataalamu wa Afya moja kutoka katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Dodoma wakifuatilia mkutano wa “Cross-Border” uliowakutanisha kujadili mikakati ya kudhibiti ugonjwa wa Kimeta, Jijini, Arusha
Baadhi ya Wataalamu wa Afya moja wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mkutano wa “Cross-Border” uliowakutanisha wataalamu hao kutoka katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Dodoma kujadili mikakati ya kudhibiti ugonjwa wa Kimeta, Jijini, Arusha.

Katika
kuhakikisha kunakuwepo na udhibiti wa ugonjwa wa Kimeta na Kichaa cha mbwa nchini wataalamu wa Afya moja
ambao ni wataalamu wa sekta za Afya ya
Binadamu, Afya ya Wanyama wafugwao na wanyamapori pamoja na sekta ya Mazingira,
wameitaka serikali kuanzisha wiki ya chanjo kwa mifugo nchini ili kuhamasisha
chanjo hizo kwa kuwa na mkakati wa pamoja na kwa wakati mmoja na hatimaye
kuweza kudhibiti maaambukizi ya magonjwa hayo kwa binadamu.
Ugonjwa huu huwapatawanyama na
binadamu kwa njia ya kung’atwa na Mbwa, Paka, Fisi au mnyama mwingine anaye
ugua kichaa cha mbwa. Ugonjwa huu hauna tiba ila unazuilika kwa njia ya chanjo.
Wakiongea
jijini Arusha wakati wa Mkutano wa
Ujirani wa kujiandaa, kujikinga na udhibiti wa magonjwa, uliowakutanisha
wataalamu hao kutoka katika mikoa ya
Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Dodoma, wamebainisha kuwa wameamua
kutoka na azimio hilo kutokana na kuwa katika baadhi ya wilaya za mikoa hiyo
milipuko ya ugonjwa wa kimeta imekuwa ikijirudia hata ndani ya
mwaka moja.
Mkurugenzi
Msaidizi, Kitengo cha Epidemiolojia na Udhibiti wa Magonjwa, Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Janneth Mghamba,amesema Wizara
imekuwa ikipokea taarifa za ugonjwa wa
Kimeta mara kadhaa katika baadhi ya Wilaya za Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro
hali inayodhihirisha hakuna mikakati ya kutosha ya udhibiti wa ugonjwa huo.
“Kinga
ni bora kuliko matibabu, hivyo ili kudhibiti haya magonjwa yanayotoka kwa
wanyama hatuna budi kujikita katika chanjo ya wanyama hao ili kupunguza
maabukizi ya wanyama hao kwa binadamu ,
Chanjo ya Kimeta na kichaa cha mbwa kwa wanyama ni ndogo kuliko matibabu
yake. Tukiwa na uhamasishaji mzuri wa chanjo na hasa kupitia hata wiki ya
chanjo, serikali itaweza kuokoa kiasi kikubwa cha fedha ambacho hutumika katika
tiba ya magonjwa hayo” Alisema Mghamba.
Aidha
Mghamba aliongeza kuwa , katika kuhakikisha kunakuwepo na mikakati ya udhibiti
wa ugonjwa huo imewakutanisha wataalamu wa afya wa mikoa husika kwa kutumia dhana ya afya moja ili waweze
kujadili kwa pamoja na kuwa na mipango ya udhibiti ya pamoja kwani magonjwa
hayana mipaka, Aidha hatua hiyo ya kuwa na mikakati ya pamoja itaweza kupunguza
gharama za udhibiti wa magonjwa.
Naye
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Dkt. Timothy Wonanji na Daktari wa wanyamaWilayani Monduli,Dkt.
Yandu Marmo wamefafanua kuwa upo
mwingiliano mkubwa wa wanyama na binadamu, katika hali hiyo uwezekano wa
magonjwa ya wanyama kuwaambukiza binadamu ni mkubwa. Aidha walieleza kuwa kukiwepo
na kampeni maalum ya kuhamasisha kuchanja wanyama kutapunguza maabukizi ya
magonjwa hayo.
Tafiti
zinaonesha kuwa asilimia 60% ya magonjwa wanayoyapata binadamu yanatoka kwa
wanyama. Kwa kulitambua hilo,Tarehe 13 Februari 2018, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa alizindua Dawati la Uratibu la
Afya moja chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, likiwa na lengo la kusimamia na
kuratibu shughuli za Afya moja nchini, Afya Moja ni dhana
inayojumuisha sekta ya afya ya binadamu , wanyamapori, mifugo na
mazingira katika kujiandaa , kufuatilia na kukabili magonjwa yanayoathiri
binadamu ,wanyamapori na mifugo.
0 Comments