Random Posts

RC Tabora: Jengeni Mazingira Mazuri ya Watoto Kujifunza

NA TIGANYA VINCENT
RS TABORA
5 May 2018
MKUU wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amewahimiza wakazi Jisesa katika Kata ya Bukuko wilayani Igunga kuhakikisha  wanaendelea kujitolea na kshiriki katika miradi ya ujenzi wa madarasa ili waweze kukamisha madarasa yaliyobaki kwa ajili ya kuweka mazingira mazuri ya watoto wao kujisomea.

Alitoa wito huo jana wilayani Igunga wakati akizungumza na wananchi wa Jisesa akiwa katika ziara ya kuhimiza mapambano dhidi ya utoro na ujenzi wa majengo ya shule yaliyo bora.

Katika kutatua tatizo la ukosefu wa madarasa na kuunga mkono juhudi hizo za wakazi wa Jisesa na Mbunge wa Jimbo la Igunga Dkt. Dalali Kafumu za ujenzi wa madarasa , Mkuu wa Mkoa wa Tabora alitoa shilingi milioni moja, Mkuu wa Wilaya ya Igunga John Mwaipopo alitoa laki tano na Halmashauri ya Igunga ilitoa milioni tano.

Hatua hiyo inalenga kuongeza nguvu ili hatimaye maboma mawili ya madarasa yalikwisha jengwa yakamilike na hatimaye na wanafunzi wawe mazingira mazuri ya kujifunza kwa ajili ya kuongeza ufaulu wao.

Shule hiyo ya Jisesa ina wanafunzi 223 ambapo zaidi ya 80 hawa madarasa ya kusomea na kulazimika kuchangia madarasa.

Hali hiyo imesababisha wanafunzi wa Darasa la VII na VI kusoma pamoja , Darasa la II, I na Chekechea nao kusoma pamoja na waliobaki kuwa hawana mahali darasa la kujisomea.

Afisa Elimu Mkoa wa Tabora Suzan Nussu alisema licha ya watoto wa shule hiyo kukosa madarasa ya kujifunzia wamekuwa miongoni shule inayofanya vizuri katika ufaulu wa mtihani wa kuhitimu darasa la saba na stadi kusoma , kuandika na kusabu(KKK).

Alisema kuwa licha ya shule hiyo inakabiliwa na uhaba wa vyumba vya madarasa imekuwa ikifanya vizuri katika mitihani yake ambapo katika mtihani wa kumaliza la saba 2017 Wilayani Igunga ilikuwa ya kwanza kwa watoto ambao darasa lina idadi ya chini ya 40.


Mkuu wa Mkoa wa Tabora ameanza ziara ya kutembelea Halmashauri zote kuhimiza vita dhidi ya utoro, mimba za utotoni na kuhimiza uibuaji wa miradi ya kilimo mashule kwa ajili ya kupata chakula cha wanafunzi 

Post a Comment

0 Comments