Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akizungumza katika Rais John Pombe
Magufuli kwenye sherehe ya kumtawaza Askofu Mkuu wa saba, Maimbo Fabian
Mndolwa, jijini Dodoma, Mei 20, 2018.2018.
(Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Askofu Mkuu wa saba wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Maimbo Fabian
Mndolwa akizungumza na waumini wa kanisa hilo na wageni waalikwa baada
ya kutawazwa kuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, jijini
Dodoma, Mei 20, 2018. Waziri Mkuu alimwakilisha Rais John Pombe
Magufuli katika sherehe hiyo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge akizungumza na Askofu
Mkuu Mstaafu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Jacob Chimeledya katika
sherehe ya kumtawaza Askofu Mkuu wa Saba wa Kanisa hilo, Maimbo Fabian
Mndolwa jijini Dodoma, Mei 20, 2018.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Askofu Mkuu wa saba wa
kania la Anglikana Tanzania, Maimbo Fabian Mndolwa baada ya ya Askofu
huyo kutawazwa kuwa Askofu Mkuu wa Kanisa hilo, jijini Dodoma, Mei 20,
2018. Waziri Mkuu alimwakilisha Rais John Pombe Magufuli.
(Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Askofu Mkuu wa saba wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Maimbo Fabian
Mndolwa akila kiapo wakati alipotawazwa kuw Askofu Mkuu wa Kanisa la
Anglikana Tanzania, jijini Dodoma, Mei 20, 2018.
(Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Spika wa Bunge Job Ndugai akisalimiana na Askofu Mkuu Mstaafu wa Kanisa
la Anglikana Tanzania , Oscar Mnunga katika sherehe ya kumtawaza
Askofu Mkuu wa Saba wa kanisa hilo, Maimbo Fabian Mndolwa jijini
Dodoma, Mei 20, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge akizungumza na Askofu
Mkuu Mstaafu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Jacob Chimeledya katika
sherehe ya kumtawaza Askofu Mkuu wa Saba wa Kanisa hilo, Maimbo Fabian
Mndolwa jijini Dodoma, Mei 20, 2018.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Askofu Mkuu wa saba wa
Kanisa la Anglikana Tanzania, Maimbo Fabian Mndolwa baada ya Askofu
huyo kutawazwa kuwa Askofu Mkuu wa Kanisa hilo, jijini Dodoma, Mei 20,
2018, kulia ni mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa. Waziri Mkuu
alimwakilisha Rais John Pombe Magufuli. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
.....................................................................................
SERIKALI imewaasa viongozi wa dini waeuepuke
migogoro ya mara kwa mara katika Makanisa yao na badala yake waendelee kuwajenga
waumini wao wakue kiroho na kujenga dhana ya umoja na upendo katika Taifa.
Pia imesema inawashukuru viongozi wa dini na
madhehebu yote ya dini kwa kuendelea kuiombea nchi amani, mshikamano na utulivu,
jambo ambalo linaongeza chachu kubwa kufikia mafanikio ya maendeleo ya kijamii,
kisiasa na kiuchumi.
Hayo yamesemwa leo (Jumapili, Mei 20, 2018)
na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika ibada ya kutawazwa Askofu Dkt. Maimbo
Mndolwa wa Dayosisi ya Tanga kuwa Askofu Mkuu wa saba wa Kanisa la Anglikana
Tanzania. Ibada hiyo imefanyika katika Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu Dayosisi ya
Central Tanganyika Jijini Dodoma.
“Nawaombeni wote kwa
ujumla wetu, tuendelee kutumia Makanisa yetu kuombea Taifa hili ili tuendelee
kuishi kwa amani, upendo na mshikamano”. Watu wa Mungu ni watu wa Upendo, watu
wa Mungu ni watu wa amani, watu wa Mungu ni watu wa kiroho”.
Waziri Mkuu ameongeza
kuwa “haitarajiwi kuona watu wa Mungu wakiwa katika mstari wa mbele kuchochea
migogoro, kuvunja amani ya Kanisa na kuongoza makundi yanayopingana katika kazi
ya Bwana”.
Amesema jukumu la makanisa
ni kuwajenga waumini kukua kiroho, na kazi ya kuwaongoza watu wamjue Mwenyezi Mungu,
ambapo amewaomba imani yao iwe moja na matendo yao yafanane na yale ya Kristo
Yesu wanayemuamini.
Waziri Mkuu amesema
kuwa nchi haiwezi kupata mafanikio ya kiuchumi na kijamii bila kuilinda amani iliyopo,
hivyo amewaomba warejee kumbusho la maandiko Matakatifu katika Waebrania
12:14 “Tatufeni kwa bidii kuwa na Amani
na watu wote”.
Pia Waziri Mkuu
ametoa wito kwa viongozi hao na wananchi kwa ujumla waendelee kuwaombea viongozi
wa Tanzania hususani Rais Dkt. John Magufuli, kuendelea kuwa na afya njema,
busara, upendo, hekima katika kuiongoza nchi yetu.
Waziri Mkuu ambaye
amemuwakilisha Rais Dkt. Magufuli katika ibada hiyo amesema Serikali inatambua
ushirikiano uliopo kati ya madhehebu mbalimbali ya dini nchini kwa ujumla wake
na kwamba ushirikiano huo ni wa kihistoria.
Amesema mara zote
madhehebu ya dini yamekuwa yakisaidiana na Serikali katika kutoa huduma za
elimu, afya, maji na makundi maalum kama vile yatima, wazee, walemavu, wajane
na huduma hizo zimekuwa zikitolewa kwa Watanzania wote bila ubaguzi wa aina
yoyote. “Mambo haya hayawezi kupatikana nchini bila ya kuwa na amani”.
Kwa upande wake
Askofu Dkt. Mndolwa baada ya kutawazwa aliahidi kulitumikia kanisa la Anglikana
katika kweli, haki na upendo.
“Naahidi kwa makini
kwamba nitaistahi na kudumisha na kuilinda Imani, haki na uhuru wa Kanisa la
Anglikana Tanzania na kulitumikia katika kweli, haki na upendo, nisijifanye
kuwa bwana juu ya urithi wa Mwenyezi Mungu, bali katika mambo yote nioneshe
kielelezo kwa kundi la Kristo. Mungu nisaidie,”.
Askofu Dkt. Mndolwa
anashika wadhifa huo baada ya aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana
Tanzania Askofu Jacob Chimeledya kumaliza muda wake. Askofu Chimeledya alitawazwa
mwaka 2013.
Maaskofu wengine
waliowahi kuongoza kanisa hilo tangu kuasisiwa kwake nchini ni John Thomas
Mhina Sepetu (1970-1978), Askofu Musa Kalemo Kahurananga (1979-1983), Askofu
John Auckland Ramadhani (1984-1997), Askofu Donald Leo Mtetemela (1998-2008),
Askofu Valentino Leonard Mokiwa (2009-2013).

0 Comments