Waziri
wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akizungumza
na wakulima wa pamba katika kijiji cha Msai wilaya ya Iramba akiwa
katika ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Singida kutembelea vituo na
kujionea ununuzi wa pamba, Picha Zote Na Mathias Canal, WK
Waziri
wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akizungumza
na wakulima wa pamba katika kijiji cha Msai wilaya ya Iramba akiwa
katika ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Singida kutembelea vituo na
kujionea ununuzi wa pamba, Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mhe
Emmanuely Lwehahula.
Kituo cha ukusanyaji na ununuzi wa pamba katika kijiji na Kata ya Msai, Wilayani Iramba
Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mhe Emmanuely Lwehahula akitoa salamu za shukrani kwa Waziri
wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba kwa kufanya ziara ya kuwatembelea
wakulima wa pamba katika kijiji cha Msai wilaya ya Iramba akiwa katika
ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Singida kutembelea vituo na
kujionea ununuzi wa pamba,
Na Mathias Canal-WK, Singida
Waziri
wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba amemuagiza Mrakibu wa polisi Wilaya
ya Iramba ASP Magoma Mtani kumkamata aliyekuwa mwenyekiti wa Bodi ya
Chama cha ushirika (AMKOS) Msai.
Waziri
Tizeba ametoa agizo hilo jana 9 June 2018 Mara baada ya kutembelea
kitongoji cha Kati, Msai na Mtoa akiwa katika ziara ya kikazi ya Siku
mbili kwa ajili ya kutembelea vituo vya ununuzi wa pamba na kujionea
msimu wa ununuzi wa zao hilo katika vijiji hivyo.
Dkt
Tizeba amelaani vikali ufujaji huo wa fedha za wakulima huku akimtaja
Paul Ramadhan Kurwa kuhusika na ufujaji huo wa shilingi milioni 23 huku
akiendelea kuonekana mtaani pasina kuchukuliwa hatua za kisheria.
"Wakati
muelekeo wa serikali yetu inayoongozwa na Rais wetu Dkt John Pombe
Magufuli ukijipambanua kutaka kuboresha maisha ya watanzania kupitia
Kilimo lakini kuna watu wanataka kurudisha nyuma juhudi hizo, hakika
tutawapa kibano kweli kweli hakuna utani kwenye fedha za wananchi"
Alikaririwa Dkt Tizeba
Mhe
Tizeba ametoa siku moja kukamatwa kwa mwizi huyo na kufikishwa
mahakamani ili awe mfano kwa wezi wengine wasio kuwa na haya wala soni.
Aidha,
amewataka wananchi katika msimu huu wa uuzaji na ununuzi wa Pamba
kutouza Pamba zenye uchafu wakidhani wataongeza idadi ya kilo kwani
kufanya hivyo ni kufifihisha juhudi zao wenyewe jambo ambalo halina
tija.
Sambamba
na hayo pia amewaondoa hofu wakulima kote nchini kuwa serikali ya awamu
ya tano inatekeleza kwa vitendo ilani ya uchaguzi ya Chama Cha
Mapinduzi yenye mkataba na wananchi katika kipindi cha miaka mitano
2015-2020.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mhe Emmanuely Lwehahula
amempongeza Waziri Tizeba kwa kutembelea maeneo mbalimbali ili kujionea
ununuzi wa Pamba huku akiwasihi wananchi wilayani humo kulima kiasi
kikubwa cha Pamba msimu ujao kwani mbegu na madawa ya kuulia wadudu
vitatolewa bure kuanzia msimu ujao wa mwaka 2018/2019.

0 Comments