Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akizungumza jambo kwenye mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Mkunguakihendo kilichopo katika kata ya Kikio, Wilaya ya Ikungi wakati wa ziara ya kukagua vituo vya ununuzi na ukusanyaji wa pamba Mkoani Singida, Jana 8 juni 2018. Picha Zote Na Mathias Canal-WK
Waziri
wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akishuhudia ununuzi na ukusanyaji wa
pamba baada ya mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Mkunguakihendo kilichopo katika kata ya Kikio, Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida, Jana 8 juni 2018.
Waziri
wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akizungumza akiwasikiliza kwa makini
maswali ya wananchi kwenye mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Mkunguakihendo kilichopo katika kata ya Kikio, Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida, Jana 8 juni 2018.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Mkunguakihendo kilichopo katika kata ya Kikio kabla ya kumkaribisha Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba , Jana 8 juni 2018.
Waziri
wa kilimo akijadili jambo na mwenyeji wake Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe
Miraji Jumanne Mtaturu akiwa katika ziara ya siku mbili mkoani Singida.
Baadhi ya wananchi wakifatilia mkutano wa hadhara
Na Mathias Canal-WK, Singida
Waziri
wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba amemuagiza Afisa ushirika wa Wilaya
ya Ikungi Mkoani Singida Ndg Gurisha Msemo kufanya ziara ya kikazi
maeneo yote kuliko fanyika uchaguzi wa viongozi wa vyama vya ushirika
ili kubaini uhalali wa uwepo wao.
Mhe
Tizeba ametoa kauli hiyo mara baada ya wakazi wa Kijiji cha
Mkunguakihendo na Misughaa Wilayani Ikungi kuonyesha kutotambua namna
walivyochaguliwa viongozi waliopo madarakani kukiongoza chama hicho
katika ngazi mbalimbali jambo ambalo lina ashiria kupatikana kwa
viongozi hao kinyume na utaratibu.
Dkt
Tizeba ameyasema hayo jana 8 Juni 2018 wakati akihutubia wananchi
waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara katika vijiji hivyo ikiwa ni
siku ya kwanza ya ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Singida.
“Pamoja
na maelekezo yangu ya kutazamwa mahali penye matatizo na kufanyika upya
uchaguzi lakini pia nawasihi pindi utakapofanyika uchaguzi mchague
viongozi waadilifu ambao watawasimamia katika kweli na haki”
“Kwa
muda mrefu sana kwenye vyama vya ushirika karibu nchi nzima watu
walikuwa wanagawana vyeo badala ya kuchagua viongozi bora kwa maslahi ya
wananchi, lakini katika kipindi hiki tumedhamiria kwa dhati kabisa kuwa
na haki katika upatikanaji wa viongozi wa chama chenu” Alikaririwa Mhe
Tizeba
Sambamba
na agizo hilo pia amewasihi viongozi mbalimbali wa vyama vya ushirika
kote nchini kutojihusisha na wizi wa fedha za wananchi kwani kufanya
hivyo sio kosa la wizi pekee bali ni kosa la uhujumu uchumi.
Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi katika mkutano huo, Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu amewasihi
maafisa ugani kuongeza ufanisi katika usimamizi kwenye kilimo ili
kuongeza tija itakayopelekea kuwa na mavuno mazuri yenye manufaa makubwa
kwa wakulima.
Aliwaomba
wataalamu wa utafiti kote nchini kupitia upya katika maeneo mbalimbali
nchini ili kubaini dawa bora za kuua wadudu wanaoathiri mazao mbalimbali
likiwemo zao la pamba.
0 Comments