Huduma za Afya ya Mama na Mtoto Dar es Salaam Yafikia Asilimia 80 - MTAZAMO MEDIA

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Thursday, 7 June 2018

Huduma za Afya ya Mama na Mtoto Dar es Salaam Yafikia Asilimia 80

 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea na baadhi ya wadau wa afya,madaktari,wauguzi na wagonjwa  hawapo pichani wakati wa ziara ya MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Hospitali ya CCBRT jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea na baadhi ya wadau wa afya,madaktari,wauguzi na wagonjwa  hawapo pichani wakati wa ziara ya MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Hospitali ya CCBRT jijini Dar es salaam.
………………………………………
Na.WAMJW-DSM
Huduma za afya ya Mama na Mtoto kwa Mkoa wa Dar es Salaam imefikia asilimia 80 ukilinganisha na miaka ya nyuma iliyopita
Hayo yamesemwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan katika ziara yake kwenye hospitali ya CCRBT leo jijiji Dar es Salaam.
“licha ya Dar es Salaam kufikia asilimia hii ni ya huduma za mama na mtoto bado tunahitaji mafunzo ya kiutendaji na kitaalam kwa watoa huduma za afya ili kupiga hatua zaidi nchi nzima”Alisema Mhe.Samia.
Hata hivyo alisema kutokana na takwimu hizo Wizara ya afya inatakiwa kufanya kazi na Ofisi ya Taifa ya Takwimu ili kupata takwimunzinazofanana kwenye utoaji wa huduma za afya nchi nzima.
Aidha,Makamu wa Rais ameipongeza hospitali ya CCBRT kwa huduma nzuri wanazozitoa hususan za wagonjwa wa Fistula kwa wanawake kwa miaka 25 nchini hivyo kuwafanya wanawake wengi kurudisha heshima na utu wao
“Hakuna jambo kubwa Duniani kama kumrudishia mtu utu na heshima kwa wanawake waliokuwa wanatenga na hata pengine kukimbiwa,kweli kazi mnayoifanya ni kazi ya Mungu” .
Kwa upande wake Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu amesema wanatambua kazi kubwa inayofanywa na wadau wakiwemo CCRBT kwa mchango mkubwa wa kutoa huduma za afya nchini ikiwemo huduma za afya ya Mama na Mtoto kwa kuwajengea uwezo watumishi wa afya nchini pamoja na kujenga vyumba vya upasuaji kwenye vituo vya afya.
“tunaposema fistula inatibika,lakini fistula inaepukika na kuzuilika pale tutakapoboresha huduma za uzazi ikiwemo huduma za dharura,nina imani wanawake wengi watajitokeza katika matibabu haya”alisema
Waziri Ummy amesema wakati serikali ya awamu ya tano inaingia madarakani kulikua na vituo vya afya vya serikali 117 sawa na asilimia 20 ambavyo vilikua vinatoa huduma ya upasuaji wa dharura nchi ilikua na vituo vya kutoa huduma ya upasuaji wa uzazi wa dharura na hadi kufikia mwezi desemba mwaka huu kutakua na vituo vipatavyo 350 sawa na asilimia 50 vya huduma hiyo vinavyomilikiwa na serikali

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages