Subscribe Us

header ads

Waziri wa Ujenzi Mhandisi Isack Kamwelwe Mgeni Rasmi Semina ya Kuwanoa Wabunifu Majengo, Wakadiriaji Majenzi AQRB

 Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) Ludigija Bulamile, (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) ofisini kwake Jijini Dar es Salaam jana kuhusina na maandalizi  semina endelevu ya kuwanoa watalaam wa  sekta ya ujenzi itakayofanyika Novemba 22-23 mwaka huu Dar es Salaam (kushoto) Kaimu Msajili wa Bodi hiyo Albert Munuo. 
PICHA NA PHILEMON SOLOMON

Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) Ludigija Bulamile, (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) ofisini kwake Jijini Dar es Salaam jana kuhusina na maandalizi kufanyika kwa semina ya kuwanoa watalaam wa  sekta ya ujenzi itakayofanyika Novemba 22-23 mwaka huu Dar es Salaam (kushoto) Kaimu Msajili wa Bodi hiyo Albert Munuo, kulia Kaimu Msaidizi wa Msajili Fedha na Utawala, Mariam Chiponde. PICHA NA PHILEMON SOLOMON

Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) Ludigija Bulamile akijibu maswali kwa waandishi wa habari. PICHA NA PHILEMON SOLOMON
Kaimu Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) Albert Munuo (aliyevaa miwani) akifafanua kuhusina na semina hiyo. PICHA NA PHILEMON SOLOMON

Na Philemon Solomon

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe,Novemba 22 anatarajia kufungua semina  ya kuwanoa Wabunifu Majengo, Wakadiriaji Majenzi na wataalamu wengine wanaoshabihiana  katika sekta ya ujenzi ili kukabiliana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia katika sekta ya ujenzi.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Kaimu Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) Albert Munuo alisema mada mbalimbali zinazohusu matumizi bora ya nishati katika majengo zitajadiliwa.

Alisema pamoja na majukumu mengine yaliyoainishwa katika kifungu cha 5 cha sheria namba 4/2010 bodi ina jukumu la kuratibu na kutoa nafasi za mafunzo endelevu kwa wadau wa sekta ya ujenzi kupitia warsha na semina mbalimbali ili kuhakikisha wataalamu wanaendana na maendeleo ya teknolojia katika kutoa huduma bora kwa jamii.

"Semikna hii ya Novemba 22 ni moja ya semina endelevu zinazotolewa na Bodi kwa  wataalamu ambapo mada mbalimbali zinazohusu matumiz bora ya nishati katika majengo,nyumba za gharama nafuu,ushindani wa kazi za kitaalamu katika soko la jumuiya ya Afrika Mashariki na ubunifu zitajadiliwa,"alisema Munuo na kuongeza kuwa wataalamu wataweza kubadilishana uzoefu wa kazi za kitaalamu kwa lengo la kuziborsha.

Pia alisema wataalamu watapata fursa ya kupata nasaha kutoka kwa viongozi mbalimbali wa serikali huku akisisitiza kwa kuwataka Wabunifu Majengo,Wakadiriaji Majenzi,Wahandisi,Wakandarasi na wadau wengine kujitokeza kushiriki katika semina hii ili kuwaongezea ujuzi na maarifa ya kuboresha utendaji kazi wao.

Aidha Bodi inawaomba waajiri wote wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi sambamba na wataamu wanaoshabihiana nao kuwafadhili kwa kuwalipia ada ya ushiriki watumishi wao na kuwaruhusu kushiriki ili waweze kuongeza tija katika utendaji kazi wao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi hiyo Ludigija Bulamile aliongeza kuwa, semina hizi ni muendelezo wa semina ambazo zilianza mwaka 2003 na hufanyika mara mbili kwa mwaka ambapo jumla ya wadau 6,403 wa sekta ya ujenzi wameweza kunufaika na mafunzo haya.

Bulamile aliongeza kwa kuipongeza serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na rais Dkt. John Magufuli kwa kutambua umuhimu wao na kuwashirikisha katika shughuli mbaklimbali za miradi ianyoendelea ukiwepo ule wa ujenzi wa reli ya kisasa SGR.

"Katika kipindi cha miaka mitatu ya rais Dkt. Mgufuli serikali imeendelea kuwatambua wataalamu wetu na kuwashirikisha katika mkradi mbalimbali ukiwepo wa ujenzi wa reli ya kisasa,"alisema Buhamile na kuongeza kusisitiza kuwataka watanzania kuwatumia waalamu hao katika ujenzi ili waweze kujenga nyumba bora zenye kuzimgatia vipato vyao.

Hata hivyo aliwaasa kuachana na dhana potofu kuwa wataalamu hao wamekuwa wakitumia harama kubwa kutoa ushauri kwa jamii kitua mbapo si cha kweli badala yake watambue kuwa wataalamu hao ni watu ambao wanarahisisha maisha kwa kshauri ujenzi kulingana na vipato vya jamii.

Post a Comment

0 Comments