Msajili
wa Bodi ya Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi Arch.Edwin Nnunduma (
wakwanza kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya mafunzo endelevu ya CPD yatakayofanyika mkoani Mwanza Desemba 2 na 3 Mwaka
huu, katikati ni Msajili Msaidizi wa Usajili na Mafunzo wa
Bodi hiyo QS. Bundala Mashaka Robaert na Mkuu wa Utawala na Fedha. Bi Mariam Chipunde.
Msajili
wa Bodi ya Wabunifu majengo na Wakadiriaji Majenzi Arch.Edwin Nnunduma (
katikati) akiendelea kuzungumza na waandishi wa habari.
Msajili
wa Bodi ya Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi Arch.Edwin Nnunduma akijibu
maswali kutoka kwa waandishi wa habari.
HABARI PICHA / NA PHILEMON SOLOMON
......................................................
Bodi ya
Wabunifu wa Majengo na Wakadiriaji Majenzi ( AQRB) imeishauri jamii
kutumia wataalamu wa ujenzi waliosajiliwa ili kusaidia miradi ya ujenzi kudumu
kwa muda mrefu nakwamba hali hiyo inasaidia kupunguza gharama za ujenzi .
Ushauri
huo umetolewa na Arch.Msajiri wa Bodi hiyo Edwini Nnunduma
wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya mafunzo
endelevu ya CPD yatakayofanyika mkoani Mwanza Desemba 2 na 3 Mwaka huu huku
Mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Gabriel Robert.
Arch.Nnunduma
amesema kwamba baadhi ya Jamii imekua ikitumia mafundi waliosomea katika
vyuo vya ufundi mbalimbali kama vile VETA katika kufanya shughuli za
ujenzi bila kutumia wataalamu wa ujenzi waliosajiliwa na bodi hiyo hali ambayo
amesema inachangia majengo mengi kutokua na ubora.
“Sisi
tunasisitiza wataalamu wetu watumike hata katika kazi binafsi,inasaidia
kufahamu ghamara za ujenzi kabla ujenzi hujaanza kufanyika,lakini pia inasaidia
kujenga nyumba zenye ubora kulingana na uwezo wa mtu kiuchumi”amesema
Arch.Nnunduma.
Kuhusu
semina ya mafunzo endelevu Nnunduma amesema kwamba Semina hiyo inatarajiwa kuwa
na washiriki wapatao 250 hadi 300 ambao ni wataalamu katika sekta tofauti
ikiwemo Wabunifu wa Majengo,Wakadiriaji wa Majenzi,Wasimamizi wa
Majengo,Wasimamizi wa Miradi na Wasamabazaji wa Vifaa vya Ujenzi.
Aidha
amesema kuwa mada mbalimbali zitajadiliwa ,ikiwemo mada kuhusu sheria mpya ya
Kodi kwenye Sekta ya Ujenzi ambapo wataalamu hao watafundishwa namna ya
kupeleka mapato TRA kwa njia ya kielektroniki kutokana na mabadiliko ya kisayansi na teknolojia.
Kwa
upande wake Msajili Msaidizi wa Usajili na Mafunzo wa Bodi hiyo Bundala
Mashaka Robaert amewaomba washiriki wajitokeze kwa wingi kushiriki semina hiyo
waweze kujengewa uelewa kuhusu mabadiliko ya teknolojia yaliyopo kwa sasa.
“Washiriki
wajitokeze kwa wingi,makampuni binafsi yawawezeshe wataalamu waweze kushiriki
semina hii ni muhimu sana manake mada ambazo tunaenda kuzijadili zitatusaidia
sana katika utendaji wetu wa kazi ,pia semina hii hufanyika mara mbili tu kwa
mwaka “amesema Msajili huyo Msaidizi.
No comments:
Post a Comment