MAAFISA JWTZ WATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI ITALIA - MTAZAMO MEDIA

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Saturday, 5 February 2022

MAAFISA JWTZ WATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI ITALIA

Maafisa Waandamizi kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wakiongozwa na Mkuu wa Kurugenzi ya Intelijensia Makao Makuu ya Jeshi, Maj. Gen. Ramadhani Mrangira pamoja na Col. Abdallah Khalfan wametembelea Ubalozi wa Tanzania Jijini Roma, Italia.

Wakiwa Ubalozini walipokelewa na mwenyeji wao Balozi wa Tanzania nchini Italia Mhe. Mahmoud Thabit Kombo ambapo pamoja na mambo megine wamezungumzia masuala ya ushirikiano. Maafisa hao walikuwepo nchini Italia kwa shughuli za kikazi. 

Balozi wa Tanzania nchini Italia Mhe. Mahmoud Thabit Kombo katika picha ya pamoja na Mkuu wa Kurugenzi ya Intelijensia Makao Makuu ya Jeshi, Maj. Gen. Ramadhani Mrangira katika ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Italia 
Balozi wa Tanzania nchini Italia Mhe. Mahmoud Thabit Kombo katika picha ya pamoja na Mkuu wa Kurugenzi ya Intelijensia Makao Makuu ya Jeshi, Maj. Gen. Ramadhani Mrangira na Col. Abdallah Khalfan 
Balozi wa Tanzania nchini Italia Mhe. Mahmoud Thabit Kombo katika picha ya pamoja na Mkuu wa Kurugenzi ya Intelijensia Makao Makuu ya Jeshi, Maj. Gen. Ramadhani Mrangira, Col. Abdallah Khalfan pamoja na baadhi ya watumishi wa Ubalozi.   

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages