| Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa Mhe. Prof. Kennedy Gaston akizungumza wakati wa kikao cha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango na wanaDiaspora wa Tanzania wanaoishi katika miji ya New York, Connecticut na New Jersey nchini Marekani iliyofanyika katika jengo la Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa jijini New York |
| Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akizungumza wakati wa kikao cha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango na wanaDiaspora wa Tanzania wanaoishi katika miji ya New York, Connecticut na New Jersey nchini Marekani iliyofanyika katika jengo la Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa jijini New York |
| Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza na wanaDiaspora wa Tanzania wanaoishi katika miji ya New York, Connecticut na New Jersey nchini Marekani katiuka hafla iliyofanyika katika jengo la Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa jijini New York |
| Balozi na Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Mhe. Dkt. Suleiman Haji Suleiman (kushoto) akifuatiwa na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Dkt. Elsie Kanza na Mkurugenzi wa Idara ya Multilateral Balozi Kahendaguza na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Marekani Balozi Swahiba Mndeme na mtumishi mwingine wa Ubalozi wa New York wakifuatilia mazungumzo ya Mhe. Makamu wa Rais Dkt. Mpango na Diaspora wa Tanzania walioko katika jiji la New York |
| Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiagana na viongozi wa Jumuiya ya WanaDiaspora wa Tanzania waishio katika miji ya New York, Connecticut na New Jersey nchini Marekani, baada ya Mazungumzo yaliofanyika katika Ukumbi wa Ubalozi wa Tanzania Jijini New York |
| Baadhi ya washiriki wa wa kikao cha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango na wanaDiaspora wa Tanzania wanaoishi katika miji ya New York, Connecticut na New Jersey nchini Marekani iliyofanyika katika jengo la Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa jijini New York |
..................................................
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isidor Mpango amekutana na Diaspora wa Tanzania waliopo katika miji ya New York, Connect Cut na New Jesry nchini Marekani na kuwasihi kuendelea kuchangia maendeleo ya nchi yao.
Mhe. Dkt. Mpango amesema kitendo cha wanaDiaspora hao na wengine walioko duniani kote kujishughulisha na shughuli za uwekezaji nchini kinaendeleza jitihada za serikali za kujikwamua kiuchumi na kuleta maendeleo ya kweli kwa wananchi wake.
''Muendelee kujishughulisha na shughuli za uwekezaji nchini kwani kufanya hivyo mnachangia maendeleo ya nchi yenu, mnaiunga mkono Serikali katika jitihada za kuleta maendeleo kwa watu wake," alisema Mhe. Dkt. Mpango.
Dkt. Mpango pia amewasihi wanadiaspora hao kufuatilia na kutumia fursa mbalimbali zilizopo nchini kwa manufaa yao binafsi, ndugu na jamaa na Taifa lao kwa ujumla.
Pamoja na mambo mengine, Dkt. Mpango amewataka wanadiaspora hao kuendelea kutafuta na kushawishi wawekezaji wengi kuja nchini na kutafuta masoko ya bidhaa mbalimbali zinazopatikana nchini na kuendelea kuisemea vizuri nchi yao ya Tanzania.
Amewapongeza Diaspora wa Tanzania kwa kuendelea kutoa mchango mkubwa wa uwekezaji hasa kupitia mfuko wa UTT Amis ambapo aliasema kuwa hadi kufikia mwaka 2021 wanadiaspora wa Tanzania walikuwa wamewekeza zaidi ya Shilingi bilioni 3.9 za kitanzania katika mfuko huo.
No comments:
Post a Comment