Habari za Hivi Punde

6/recent/ticker-posts

Header Ads Widget

BALOZI WA SANTA MIZAWADI WA AIRTEL ATANGAZA ZAWADI HADHARANI

Balozi wa Santa Mizawadi wa Alrtel Tanzania, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari wakati akitaja zawadi mbalimbali zitakazo tolewa kwa washindi wa promosheni ya Santa Mizawadi na droo ya kwanza ambayo itafanyika jumanne.

................................

Na Phabyola Sumary , Dar es Salaam

SANTA Mizawadi  wa Alrtel  amezitangaza zawadi  zitakazotolewa  kwa wateja na mawakala wote watakaoshiriki promosheni ya Santa Mizawadi inayoendeshwa na Airtel Tanzania katika kipindi hiki cha Sikukuu.

Promosheni hiyo ambayo imezinduliwa hivi karibuni imelenga kutoa shukrani na kuwazadia wateja na mawakala wote wanaoendelea kutumia huduma za Airtel katika  kipindi hiki cha sikukuu.

Droo ya kwanza ya Promosheni hiyo inatarajiwa kufanyika Desemba 24, 2025 siku ya jumanne ambapo washindi watakaopatikana wanajinyakulia mizawadi hiyo.

Balozi wa Alrtel Mr Santa alitaja baadhi ya zawadi zitakazotolewa kuwa ni pocket WiFi, simu janja, pikipiki, runinga na pesa Taslim hadi shilingi milioni moja.

Akizungumziaa  promosheni hiyo ya  Airtel Santa Mizawadi, Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, Jackson Mmbando alisema Promosheni ya Airtel Santa Mizawadi lengo  lake kubwa ni kuwashukuru wateja na mawakala waaminifu hasa wale wanaoendelea kutumia bidhaa za kampuni hiyo.

Akielezea jinsi ya kushiriki na kujishindia Mizawadi ya Airtel Santa Mizawadi, Mmbando alisema  mshiriki aatakiwa kufanya miamala ya kuweka na kutoa fedha, ambapo pia ili mteja aweze kuingia kwenye droo anatakiwa kufanya miamala kama vile kununua bando, Kutuma pesa, kutoa pesa, kulipa bili, kufanya miamala ya kibenki, kutuma au kupokea pesa nje ya nchi, kununua muda wa maongezi au vifurushi kupitia *149*99#, *150*60#, au kwa kutumia ‘My Airtel App’.

Meneja Huduma kwa Wateja, Celine Njuju alisema kampuni hiyo inawathamini  wateja wake na kueleza kuwa kila wiki watachezesha droo kwa ajili ya kuwapata washindi na watapigiwa simu kwa namba 100 namba ambayo imekuwa ikitumiwa na kampuni hiyo kwa mawasiliano.

Balozi wa Alrtel Mr Santa  akicheza wimbo wa Chrismas wakati akihamasisha promosheni hiyo. Wanaofurahia tukio hilo kutoka kushoto ni Meneja Huduma Kwa Wateja, Celine Njuju na Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, Jackson Mmbando.
Meneja Huduma Kwa Wateja, Celine Njuju akizungumza.
Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, Jackson Mmbando akizungumzia promosheni hiyo.
 

Post a Comment

0 Comments