Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando akizungumzia kuhusu droo hiyo.
.................................
Na Phabyola Sumary, Dar es Salaam
MJASIRIAMALI wa
kushona nguo Fatuma Mwandege mkazi wa Ukonga Majumba Sita jijini Dar es Salaam
amepata zawadi ya pikipiki baada ya kuibuka kidedea katika promosheni inayo
endeshwa na Airtel Tanzania ya Santa Mizawadi.
Mwandege amepata
zawadi hiyo pamoja na wenzake ambao wameshinda zawadi mbalimbali zikiwemo
runinga, simu janja, pocket WiFi, fedha taslim
Sh.Milioni 1 na nyingine nyingi.
Mwandege
ameishukuru kampuni hiyo ya simu kwa kuendesha promosheni hiyo kwa ajili ya
wateja wake na mawakala ambao wanakwenda kuongeza kasi ya kutumia huduma
mbalimbali za Airtel.
Mwanamke huyo na
wenzake wamejinyakulia zawadi hizo katika droo ya kwanza ya promosheni hiyo
ambayo iliyofanyika jana jijini Dar es
Salaam na kuhudhuriwa na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali.
Wengine
waliojishindia zawadi mbalimbali ni pamoja na Andrew Chiomo mwendesha bodaboda
mkazi wa Ifakara mkoani Morogoro aliyepata fedha taslimu Sh. Milioni 1,
Josephine Mgalu mkazi wa Nzega ambaye alijishindia pocket Wifi.
Aidha, washindi
wengine ni Omari Ramadhani mkazi wa Shinyanga ambaye amepata simu aina ya smart
phone na Halima Kimaro ambaye naye ni mkazi wa Shinyanga ambaye alijishindia
Runinga inchi 55 na washindi wengine ambao walijinyakulia zawadi za aina
tofauti tofauti.
Akizugumza
wakati wa promosheni hiyo Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo,
Jackson Mmbando alisema promesheni hiyo inaendelea hadi mwezi Januari mwakani na kuwa
itakuwa ikifanyika kila wiki.
Amesema
Airtel Santa Mizawadi ni promosheni ambayo imelenga kutoa shukurani kwa wateja
wao na mawakala ambao wanaendelea kutumia huduma za kampuni hiyo.
Mmbando
alitaja zawadi zinazotolewa kwa washindi hao kuwa ni pocket WiFi, simu janja,
pikipiki, runinga na pesa Taslim Shilingi milioni moja.
Alisema
jinsi ya kushiriki na kujishindia
mizawadi hiyo wateja wao na mawakala wanatakiwa kufanya miamala ya kuweka na
kutoa fedha, ambapo pia ili Mteja aweze kuingia kwenye droo anatakiwa kufanya
miamala ya kununua bando, Kutuma pesa,
kutoa pesa, kulipa bili, kufanya miamala ya kibenki, kutuma au kupokea
pesa nje ya nchi na kununua muda wa
maongezi.
0 Comments