Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa meza kuu na viongozi mbalimbali kwenye Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika kuhusu Mpango wa Maendeleo ya Kilimo Afrika uliofanyika Kampala Uganda Januari 11, 2025.
.......................................
Na Mwandishi Wetu, Uganda
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Januari 11, 2025 ameshiriki Mkutano Maalum
wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa
Afrika kuhusu Mpango wa Maendeleo ya Kilimo Afrika ambapo alimwakilisha Rais
Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mkutano huo uliofanyika kwenye Kituo cha
Mikutano cha Speke Resort, Munyonyo, Kampala Uganda.
Awali Mheshimiwa Majaliwa alishuhudia
Tamasha la Kahawa Afrika (Africa Coffee Festival) lililolenga
kuhamasisha uongezaji thamani katika mazao yanayolimwa Afrika
likiwemo zao la kahawa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa kwenye mkutano huo.
Washiriki wakiwa kwenye mkutano huo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishiriki kwenye mkutano huo.
Wimbo wa Afrika Mashariki ukiimbwa.
0 Comments