Random Posts

DKT. MWAMBA ATETA NA BALOZI WA JAPAN

Kikao kikiendelea kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Yoichi Mikami, ambaye alifika ofisini kwake kujitambulisha na kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya pande hizo mbili.

Na. Josephine Majura WF, Dodoma

Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha Dkt. Natu El-maamry Mwamba, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Yoichi Mikami, kilichofanyika jijini Dodoma, ambapo walijadili namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika nyanja mbalimbali za kiuchumi na kijamii. 

Dkt. Mwamba, aliishukuru Serikali ya Japan kwa kuendelea kuwa wadau muhimu wa maendeleo ya nchi.

Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Kamishna wa Sera Wizara ya Fedha, Dkt. Johnson Nyella, Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. Melckezedeki Mbise, Mchumi kutoka Wizara ya Fedha Bw. Edson Vedasto na Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Robert Bendera.

Post a Comment

0 Comments