Jeshi la
Polisi nchini limesema linaendelea na mikakati ya kutumia mifumo mbalimbali ya
kielektroniki iliyoanzishwa na serikali, ambayo itasadia kuleta uwazi,
uwajibikaji na udhibiti wa matumizi ya fedha za umma.
Hayo
yamesemwa na Kamishna wa Fedha na Lojistiki wa Jeshi la Polisi, CP Liberati
Sabas wakati akifungua kikao kazi cha Maafisa Wanadhimu na Wahasibu wa Jeshi la
Polisi kutoka Makao Makuu, Mikoa, Vikosi na Vyuo, katika shule ya Polisi
Tanzania (TPS - Moshi ) mkoani Kilimanjari Machi 14, 2025.
CP Sabas
amewataka Maafisa wanadhimu na Wahasibu kwenda kuwajibika ipasavyo katika
maeneo yao ikiwa ni pamoja na kuwasimamia watendaji wa chini yao kutumia vyema
mifumo hiyo sambamba na kusimamia fedha zote ambazo ziliainishwa na serikali
kwa mwaka wa fedha 2024/ 2025 kwa kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma.
Kikao kazi cha Maafisa Wanadhimu na Wahasibu wa Jeshi la Polisi kutoka Makao Makuu, Mikoa, Vikosi na Vyuo hufanyika kila mwaka kwa lengo la kujadili mambo mbalimbali yanayohusu masuala ya usimamizi wa rasilimali fedha ndani ya Jeshi la Polisi.
No comments:
Post a Comment