.....................................
Na Christopher Siwingwa -Dar es salaam
Watanzania wametakiwa kununua na kuthamini bidhaa zinazotengezwa na Viwanda vya ndani.
Tanzania ina Viwanda ambavyo vinazalisha bidhaa bora na zenye viwango vya kimataifa, lakini watanzania wengi hawavithamini na kukimbilia kununua bidhaa za nje.
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Suleiman Jafo amesema hayo wakati wa hafla ya futari mlimani city jijini Dar es salaam ilioandaliwa na kampuni ya ujenzi ya Magic Builders International.
Dkt Jafo amewataka wadau wa wa ujenzi kujijengea uwezo binafsi utakaowawezesha kishiriki katika uwakilishi wa medani tofauti za za ujenzi wa ndani na nje ya nchi,na hatime kufika nafasi za juu kwenye uzalishaji ili kulinda na kuongeza thamani bidhaa za ndani.
Nae mmoja wa wakurugenzi wa kampuni ya ujenzi ya Magic, bwana David Barongo ameipongeza serikali kwa kufanya mageuzi ya Viwanda vya ndani ambayo imewapa motisha kuendelea kuzalisha bidhaa zenye viwango vya kimataifa .
Bwana Barongo amesema tunajivunia kampuni yao kuwajali wadau wa sekta ya ujenzi na ndio maana inakutana nao mara kwa mara ili kupeana uwezo na kutatua changamoto mbali mbali zinazowakabili.
Pia amesema wanatambua mchango mkubwa wa serikali ya Dkt Samia Suluhu Hassan inaotoa kwenye sekta ya ujenzi ambayo imewapa motisha kuendelea kuzalisha bidhaa zenye viwango.
No comments:
Post a Comment