DC NYAMWESE AKAGUA UJENZI WA CHUO CHA VETA HANDENI - MTAZAMO MEDIA

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday, 26 September 2025

DC NYAMWESE AKAGUA UJENZI WA CHUO CHA VETA HANDENI

Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mhe. Salum Nyamwese, akikagua ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) wilayani humo.

............................... 

Na Mwandishi Wetu, Handeni

MKUU wa Wilaya ya Handeni, Mhe. Salum Nyamwese, amekagua ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) wilayani humo na kuagiza maboresho mbalimbali kwenye utekelezaji wa mradi huo unaotarajiwa kugharimu Sh.Bilioni 1.6.

Miongoni mwa maboresho ni kuangalia namna ya kuhakikisha bweni linajumuishwa katika awamu ya kwanza ya ujenzi, ili wanafunzi waweze kuanza kupata mafunzo mara tu awamu hiyo itakapokamilika.

Akizungumza baada ya kukagua mradi huo, Nyamwese amewataka mshauri elekezi na msimamizi wa mradi kushirikiana kuhakikisha bweni linaingizwa katika mpango huo kutoka na awamu ya kwanza inayohusisha majengo tisa kutokuwa na bweni.

Vilevile, ameelekeza Jeshi la Zimamoto lishirikishwe mapema kutoa ushauri kuhusu vifaa vya usalama vinavyohitajika kabla ya mradi kukamilika.

Hata hivyo, amewapongeza wasimamizi wa mradi kwa kazi nzuri iliyofanyika, akisisitiza mapungufu yaliyojitokeza yashughulikiwe mara moja.

Ukaguzi wa ujenzi wa chuo hicho ukiendelea
Muonekano wa moja ya majengo ya chuo hicho.
Muonekano wa moja ya majengo ya chuo hicho.

Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mhe. Salum Nyamwese akitoa maelekezo baada ya kukagua ujenzi huo.

 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages