Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Jacob John Mkunda, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuliwezesha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa zana na vifaa vya kisasa vinavyoliwezesha kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.
Jenerali Mkunda ametoa shukrani hizo katika hafla ya kuwapongeza wanamichezo wa Timu ya Kanda ya Ngome, iliyofanyika baada ya kumalizika kwa Mashindano ya Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMMATA) 2026 yaliyofanyika jijini Mwanza.
Aidha, hafla hiyo ilipambwa na burudani mbalimbali kutoka kwa vikundi vya sanaa, sarakasi na muziki wa dansi vya Mwenge pamoja na Kimbunga JKT Mgulani, vilivyowaburudisha washiriki na wageni waliohudhuria hafla hiyo.





0 Comments