Uzinduzi
wa shindano la Big Brother Africa umefanyika usiku huu katika ukumbi wa
Samaki Samaki City Centre maeneo ya Posta jijini Dar es salaam ambapo
wawakilishi wa tamasha hilo kutoka mataifa mbalimbali barani Afrika
wamewekwa hadharani.
Uzinduzi
huo umeoneshwa moja kwa moja na rununga ya DSTV huku Bi.Feza Kessiy na
Ammy Nando wakitajwa kuwakilisha Tanzania katika msimu wa nane wa Big
Brother Africa.
Kwa
hapa Tanzania uzinduzi huo ulidhaminiwa na kampuni ya simu za mkonono ya
Airtel ambapo wametoa zawadi mbalimbali zilizoshindaniwa na watu
waliohudhuria katika zoezi hilo.
Burudani kubwa ya muziki ilitawala katika ukumbi huo ambapo wageni waalikwa wamefurahi pamoja kwa kula na kunywa.
Kutoka
kushoto ni Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya MultiChoice Tanzania,
Furaha Samalu, (katikati) meneja rasilimali watu wa Multi Choice Tike
Mwakitwange, wa kwanza kulia ni Meneja uhusiano wa Multi Choice
Barbara Kambogi wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa Uzinduzi wa Big
Brother Africa katika ukumbi wa Samaki Samaki City Centre maeneo ya
Posta jijini Dar es salaam usiku wa leo
Mhudumua
wa kampuni ya simu ya Airtel ambao ni wadhamini wa Uzinduzi wa Big
Brother Africa mwaka huu (mwenye T-shirt nyekundu) akiwahudumia wateja
wanaotaka kusajili namba zao pamoja na kujiunga na huduma ya Airtel
Money wakati wa tamasha hilo
Meneja
uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi (kulia) akizungumza
na wageni waalikwa , waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa Big Brother
Africa , pamoja na huduma za MultiChoice kwa wateja wake
Balozi
wa Airtel Tanzania, msanii wa muziki wa kizazi kipya, Ambwene Yesaya AY
akikabidhi kadi ya mwaliko mara baada ya kuingia katika ukumbi wa
Samaki Samaki City Centre
Wasanii
kutoka Afrika kusini wakiburudisha watu katika runinga ya DSTV wakati
wa uzinduzi wa Big Brother Africa leo katika ukumbi wa Samaki Samaki
City Centre maeneo ya Posta jijini Dar es salaam
Wadau
mbalimbali waliohudhuria katika uzinduzi huo wakifuatilia matangazo ya
kituo cha televisheni cha DSTV kinachoonesha matangazo hayo moja kwa
moja
Mshindi
wa zawadi ya simu aina ya Samsung Galaxy, bwana Dennis Fussi kutoka
Magazeti ya Daily News na Habari Leo. Zawadi hiyo imetolewa usiku huu
kutoka kampuni ya simu za mkonono inayoongoza kutoa huduma bora ya
Airtel katika Ukumbi wa Samaki Samaki City Centre maeneo ya Posta jijini
Dar es salaam
(PICHA ZOTE NA BERNARD JAMESI WA MTAZAMO MEDIA GROUP)
0 Comments