Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe Dar es salaam
Wagosi
wa kaya wanaendelea kujifua katika dimba la CCM Mkwakwani jijini Tanga
kuelekea msimu mpya wa ligi kuu soka Tanzania bara unaorajia kuanza
kushika kasi Agosti 24 mwaka huu huku malengo yao yakiwa ni kutwaa
ubingwa.
Akizungumza mchana huu na mtandao wa FULLSHANGWE
kwa njia ya simu kutoka Tanga, Kocha mkuu wa klabu hiyo, Mzanzibar,
Hemed Morocco amesema kikosi chake kinaendelea kuimarika kadri siku
zinavyozidi kuyoyoma, huku akiwasifu wachezaji wake kushika haraka
maelekezo yake.
“Tumesajili
wachezaji wapya, lakini wapo wa zamani, najisikia vizuri sana kuona
wachezaji wangu wanaelewa kwa haraka kile ninachohitaji mimi. Ingawa
bado ni mapema sana na siwezi kuahidi makubwa, lakini kikosi changu
kinatia matumaini na kunipa cha kuzungumza”. Alisema Morocco.
Morocco
alisema baada ya kucheza mechi za kirafiki ikiwemo ile ya Simba ambayo
walishinda kwa bao 1-0 uwanja wa Mkwakwani, amebaini baadhi ya makosa na
hivi sasa anajitahidi kuyafuta kwa kiasi kikubwa hususani safu ya
ushambuliaji.
“Toka
msimu uliopita, safu yangu ya ushambuliaji haikuwa nzuri sana, lakini
hili ni tatizo la taifa zima, ni ukweli usiofichika kuwa timu nyingi
zina matatizo ya ushambuliaji, ila ninajitahidi sana angalau kunoa safu
yangu ili iwe na makali kabla ya kuanza ligi kuu”. Alisema Morroco.
Kocho
huyo anayesifika kufundisha soka safi, aliwasifu wachezaji wake wapya
Kenneth Masumbuko, Juma Nyoso, Haruna Moshi “Boban”, Crispin Odula kwa
uwezo mkubwa waouonesha wakiwa uwanjani.
“Hakika
vijana hawa ni faraja kubwa kwangu, kila kukicha wanacheza mpira mzuri
mno, naamini nitafanikiwa ndoto zangu. Ila kwa mashabiki wetu, nawasihi
wasiwe na haraka, bado ni mapema, lakini nahitaji ushirikiano kutoka
kwao”. Alisema Morroco.
Wagosi
wa Kaya wataanza kampeni ya kutafuta ubingwa wa ligi kuu soka Tanzania
bara Agosti 24 ambapo wataanzia ugenini dhidi ya JKT Oljoro katika dimba
la Sh. Amri Abeid Kaluta mjini Arusha.
0 Comments