Rais
Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi
Mhe. James Mbatia na daktari wa zamu wakimwangalia Mjumbe wa Tume ya
Katiba Dkt. Sengondo Mvungi alipokuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa
ya Muhimbili kitengo cha Mifupa (MOI) Oktoba 3, 2013 kufuatia
kujeruhiwa kwake na watu wanaosadikiwa ni majambazi usiku wa Jumamosi
Oktoba 2, 2013.
(PICHA NA IKULU)
TAARIFA
ZILIZOTUFIKIA KITENGO CHA HABARI KATIKA MTANDAO WAKO WA
www.fullshangweblog.com ZINASEMA KUWA MJUMBE WA TUME YA KATIBA
ALIYEJERUHIWA NA WATU WANAOSADIKIKA NI MAJAMBAZI USIKU WA JUMAMOSI
OKTOBA 2 MWAKA HUU, DKT. SENGONDO MVUNGI , AMEFARIKI DUNIA LEO ALASIRI
NCHINI AFRIKA KUSINI ALIPOKUWA AKITIBIWA.
MWENYEKITI
WA CHAMA CHA NCCR-MAGEUZI NA MBUNGE WA KUTEULIWA MHE. JAMES MBATIA
AMETHIBITISHA KUTOKEA KWA KIFO HICHO CHA DKT. MVUNGI ALIYEWAHI KUWA
KIONGOZI MKUBWA WA CHAMA HICHO.
KITENGO CHA HABARI KINAFUATILIA KWA KINA TAARIFA HIZO, TAFADHALI ENDELEA KUWA NASI.
CREW NZIMA YA MTANDAO HUU INATOA POLE KWA WATANZANIA WOTE WAKATI HUU WA MAJONZI.
MWENYEZI MUNGU AWAPE NGUVU.
AMINA
0 Comments