Random Posts

MACHINGA NA BODABODA WAENDELEA KUKAIDI AMRI YA MKUU WA MKOA NA JIJI

                                                     Na-Bernard James
                                                           ................


Wamachinga yaani wale wafanya biashara ndogondogo  wasio na sehemu maalumu ya kufanyia biashara,na Bodaboda`inaonekana wamepuuza amri ya Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam na halimashauli za jiji ya kuwapiga marufuku  kufanya   biashara sehemu ,ambazo sio rasmi na kwenda katika maeneo yaliyotengwa maalum kwa ajili  ya biashara zao.hii imejidhihilisha hivi leo maeneo ya kariakoo,wamachinga wamerudi tena nakufanya mitaa ya kongo kuwa napurukushani.pamoja na wamachinga kurudi kinyemela kariakoo,nao askari wa jiji wamewafanya machinga kama ndio mradi wao wa kujiingzia pesa haram ,wamekuwa wana wakamata nakuwaomba pesa kuanzia elfu 10 ,hivyo kufanya zoezi lilliotangazwa na mkuu wa mkoa .kuwa gumu wakati lilikuwa ni rahisi.
Hali ya rushwa nchini imekuwa ni donda ndugu.pamoja na Mhe Rais kulivalia njuga kulikomesha ,Tatizo ni wale waliokabiziwa jukumu la kulishugulikia
Nao polisi wa barabarani na ulinzi shilikishi wamefanya bodaboda mradi,
Bodaboda wameamua makusudi kuvuruga utaratibu waliowekewa wakuto kuingia katikati ya jiji kinyume kabisa tena kwa jeuri ,wanaingia katika ya jiji nakusababisha ajari nyingi,na hawafati utaratibu imekuwa ni fujo na kero .Polisi wa barabarani wanawakamata na kuwaachia katika mazingila ya kutatanisha,bado kuna haja ya  serikali kuwaangalia kwa jicho la umakini bodaboda kwa kuwachukulia hatua kali zaidi ,hakuna kitu kinachoshindikana mbona Waziri wa uchukuzi Mhe Dk Mwakyembe ameweza kumaliza,kero zilizo kuwa zinatokea bandarini?aliuliza Jumanne Hasani mkazi wa ilala.