Random Posts

MKE WA WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA MAMA DORCAS MEMBE AFUNGUA KITUO CHA KUSAMBAZIA MATREKTA WAKULIMA CHA KARIATI MATRACTOR KILICHOPO KINONDONI DAR ES SALAAM AGOSTI 20, 2014

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Kusambaza Matrekta kwa Wakulima ya Kariati Matractor , Omary Kariati (kulia), akimkaribisha mgeni rasmi Mke wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikianmo wa Kimataifa, Mama Dorcas Membe wakati akiwasili katika hafla ya kufungua kituo hicho kilichopo Kinondoni Dar es Salaam leo asubuhi.
PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE 
.............................................
 Mke wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikianmo wa Kimataifa, Mama Dorcas Membe (katikati), akisalimiana na Meneja wa Uhusiano kwa Wateja Wakubwa wa Benki ya KCB, Victor Malewo, ambapo wamekiwezesha kituo hicho kupata mikopo ya kununulia matrekta hao.
 Mke wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikianmo wa Kimataifa, Mama Dorcas Membe na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Kusambaza Matrekta kwa Wakulima ya Kariati Matractor , Omary Kariati wakionesha tovuti ya kituo hicho baada ya kufungulia. Tovuti hiyo ya www.kariatimatractor.com itamsaidia mkulima yeyote aliopo nchini kupata fomu kwa ajili ya kununua matrekta hayo.
 Mke wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikianmo wa Kimataifa, Mama Dorcas Membe (katikati), akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Kituo cha Kusambaza Matrekta cha Kariati Matractor kilichopo Kinondoni Dar es Salaam jana. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo hicho, Omary Kariati na Meneja wa Uhusiano kwa Wateja Wakubwa wa Benki ya KCB, Victor Malewo, ambapo wamekiwezesha kituo hicho kupata mikopo ya kununulia matrekta hayo.