Afisa Masoko wa Kampuni ya Hotpoint Tanzania ambao ni wasambazaji wa Bidhaa za LG, Grace Kavishe, Carolyn Jesse akiongea na waandishi wa habari kuwaelezea jinsi jokofu hilo linavyoweza kufanya kazi.
Na Bernard James
+255752106535
..................
Kampuni inayo sambaza na kuuza vifaa bora kabisa
vya umeme nchini,Kampuni ya LG,Imezindua vifaa vya Umeme jijini Da Es Salaam
katika Hotel ya New Afrika leo imezindua jokofu la kisasa yenye uwezo wa
kutunza ubaridi kwa muda wa masaa saba upande wa jokofu ya kawaida na masaa
kumi kwa upande wa friza hata pindi umeme unapokuwa umekatika.Vifaa vyote
vinavyosambazwa na kuuzwa na LG ni imara na haviigwi ,hakuna bidhaa feki za LG
hapa nchini ambazo wafanya biashara wasio waaminfu wanaotumiaga ujanja
wakuingiza bizaa fake ,wakati sio halisi wameweza kuingiza nchini ,LG ni
kampuni ambayo imefanikiwa kulinda ubora wake halisi.
Bidhaa hii mpya imezinduliwa mahususi kutokana na
tatizo lililo kithiri la katizo la umeme ambalo hukumba maeneo mengi ya nchi na
kusababisha vifaa vya umeme kukosa matumizi kwa muda mrefu.na kuungua,hivyo
kusababisha hasara kwa mtumiaji.
Aidha tatizo hili la kukatika kwa umeme mara kwa
mara kumepelekea makapuni kama LG kutanua wigo wao katika kutafuta suluhu na
hivyo kubuni teknolojia zenye usasa uliopindukia katika ubunifu wa vifaa
vitavyo himili nyakati umeme unapokosekana. Ni katika ubunifu huo ndipo LG
ikatengeneza jokofu hili jipya lisilogandisha barafu kwenye “friza” linaloweza
kutunza ubaridi katika sehemu ya ‘friji” kwa zaidi ya masaa saba hasa pale
umeme unapokatika kwa kipindi kirefu.
Akiongea siku ya uzinduzi Appliances Product
Manager LG East Africa, Oktae Kim alisema uzinduzi huu umelenga katika ubunifu
mkubwa unaohusiana na mahitaji ya mteja na jinsi ya kuyatatua. Hivyo basi
tunajitahidi kubuni bidhaa ambazo zina kidhi mahitaji ya wateja wetu.
Teknolojia iliyotumika inahusianisha valve kwenye
jokofu ambayo hufunguka pale ambapo kunapokosekana na umeme. Valve hii inasambaza
ubaridi kwenye vifaa vingine vilivyoundwa maalumu kutunda ubaridi na pindi
umeme ukatikapo vipaa hivi huanza kutoa ubaridi kwa muda wa saa saba.
Bwana Kim amesema: “Evercool inapooza mara tatu
zaidi kwa kutumia evaporator tatu. Evaporator kuu inatumia umeme na mbili
zinafanya kazi bila kutumia umeme. Kwa hiyo sasa unaweza kufaidi vinywaji
baridi na kuepuka kuharibika kwa chakula chako kwenye jokofu mara umeme
unapokatika”.
LG ina visahani vya kugandishia barafu ambavyo vina
uwezo wa kugandisha barafu kwa haraka ya zaid ya asilimia 20. Imetengenezwa kwa
umahiri na maeneo ya kutosha kwa ndani na hivyo kukuwezesha kupata sehemu ya
kutosha ndani wakati wa kuweka vitu. Sasa unaweza kutunza mboga na matunda
vizuri bila kuogopa vitu kuharibika kutokana na mrudikano wa vitu nahivyo
kusababisha unyevunyevu unaopelekea kuharibu vyakula. Na wakati wa kipindi cha
joto kali, jokofu hili la milango miwili litakushangaza kwa kutunza chakula kwa
hali ya juu.
Pia mwanga wa LED unang’aa zaidi, unadumu kwa muda
mrefu na unatumia umeme mdogo. Na mtu atakayenunua jokofu hili hahitaji
kutafuta ‘Stabilizer” kwani jokofu hili linaweza kufanya kazi vizuri hata
wakati umeme unapokuwa mdogo.
Bw. Kim aliongezea kwakusema :compressor za LG ni
Imara na tunakupa guarantee ya mwaka mzima” Pia aliongeza kuwa wanajitahidi
kuhakikisha wanaendelea kuzalisha bidhaa za kisasa na zinazoendana na mahitaji
halisi ya watu.
|
0 Comments