Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Morrice Oyuke akizungumza katika mkutano na wanahabari Dar es Salam leo asubuhi kuhusu pato la Taifa kwa robo ya pili ya mwaka kuanzia Aprili hadi Juni-2014.
Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Morrice Oyuke (kushoto), akizungumza katika mkutano na wanahabari Dar es Salam leo asubuhi kuhusu pato la Taifa kwa robo ya pili ya mwaka kuanzia Aprili hadi Juni-2014. Kulia ni Mtakwimu Mwandamizi, Jovita Rugemalira na Mtakwimu Mkuu Uchumi, Adela Ndesangia.
Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Morrice Oyuke (wa pili kushoto), akizungumza katika mkutano huo. Kushoto ni Mtakwimu Mkuu Uchumi, Fred Matola. Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.
Dotto Mwaibale
SEKTA ya kilimo na uvuvi imeongeza pato la taifa kwa asilimia
5.4 ukilinganisha na asilimia 4.9 kwa mwaka 2014.
Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Morrice Oyuke Dar es Salaam
jana wakati akizungumza katika mkutano na wanahabari
kuhusu pato la taifa kwa robo ya pili ya mwaka kuanzia Aprili
hadi Juni-2014.
Alisema katika kipindi hicho shughuli za kilimo na mazao
zilikuwa kwa asilimia 6.5 mwaka huu ukilinganisha na asilimia
5.3 mwaka 2013 na kuwa shughuli za mifugo zilikuwa kwa
asilimia 0.9 mwaka 2014 ikilinganishwa na asilimia 3.8.
Oyuke alisema shughuli za misitu na uwindaji zilikua kwa
asilimia 0.8 mwaka huu ikilinganishwa na asilimia 3.2 kwa
mwaka 2013.
Alisema katika Sekta ya viwanda na ujenzi shughuli za
uchimbaji madini, mawe na kokoto ziliongezeka na kufikia kasi
ya asilimia 3.0 katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka huu
ilikilinganishwa na kasi ya ukuaji wa asilimia hasi 6.2 katika
kipindi kama hicho kwa mwaka 2013.
Oyuke alisema kuongezeka kwa kasi hiyo kulitokana na
uzalishaji wa madini ya almasi na Tanzanite katika robo ya pili ya mwaka huu.
Hata hivyo Ayuke alisema uzalishaji wa dhahabu ulipungua
katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka 2014.

0 Comments