Daktari bingwa wa upasuaji wa watoto katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH, Dk Victor Ngotta (kushoto) akimfanyia
upasuaji Eliudi LEO kwa kushirikiana na Profesa Saber Waheeb (katikati) na Dk
Mohamed Malak kutoka Misri (kulia).
Dk Mohamed
Malak, Profesa Saber Waheeb kutoka Misri na Dk Victor Ngotta wakiendelea na
upasuaji LEO katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
Daktari Bingwa Watoto wa Upasuaji, Dk
Zaituni Bokhary akizungumza jambo baada ya kumfanyia upasuaji mtoto Elikana aliyekuwa
na tatizo la mfumo wa njia ya mkojo Leo.
Dk Bingwa wa Upasuaji, Dk Yona Ringo akiwa
ofisini baada ya kumfanyia upasuaji mtoto Elikana ambaye alikuwa na tatizo la mfumo
wa njia ya mkojo Leo.
..............................................................................
Na John Stephen
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
(MNH) LEO imefanikisha kuwafanyia upasuaji watoto pacha ambao walikuwa wana
tatizo katika njia mkojo.
Watoto hao wametoka katika chumba
cha upasuaji salama na sasa wanaendelea vizuri baada ya kurejeshwa wodini.
Watoto hao ni Eliudi Joel na Elikana Joel ambao wana umri wa miaka mitatu kila
mmoja.
Daktari Bingwa Watoto wa Upasuaji,
Dk Zaituni Bokhary na Dk Bingwa wa Upasuaji, Dk Yona Ringo wamefanikisha
upasuaji wa Elikana wakati Eliudi amefanyiwa upasuaji na Profesa Saber Waheeb
na Dk Mohamed Malak kutoka Misri kwa kushirikiana na Dk Victor Ngotta na Dk
Mwajabu Mbaga wa Muhimbili.
Dk Bokhary amesema kuwa upasuaji wa
watoto hao umechukua saa moja na nusu na kwamba hivi sasa wanaendelea vizuri
baada ya shughuli hiyo.
“Watoto hawa wataendelea kuwapo
wodini hadi watakapopona vizuri ndio tutawaruhusu,” amesema Dk Bokhary.
Dk Bokhary amesema kuwa watoto
wengine wawili leo wamefanyiwa upasuaji ambao walikuwa na tatizo kama hilo.
Jana madaktari wa hospitali hiyo
walianza upasuaji kwa watoto wenye matatizo ya njia ya mkojo na mfumo wa hewa
na chakul



