Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Balozi wa India hapa nchini Sandeep Arya
mara baada ya kupokea mfano wa hundi yenye thamani ya Shilingi za Kitanzania
milioni 545 Ikulu jijini Dar es Salaam. Msaada huo umetolewa na Serikali ya
India kwa ajili ya kuwasaidia waathirika
wa Tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera. Wakwanza (kushoto) ni Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akiwa pamoja na Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje Balozi Dkt.
Aziz Mlima wakishuhudia tukio hilo.
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akiwa anatazama mfano wa hundi hiyo na Balozi wa India
hapa nchini Sandeep Arya pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Balozi wa India hapa nchini Sandeep Arya mara
baada ya kupokea mfano wa hundi yenye thamani ya Shilingi za Kitanzania milioni
545 Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo kwa furaha na Balozi wa India hapa
nchini Sandeep Arya mara baada ya kupokea mfano wa hundi yenye thamani ya Shilingi
za Kitanzania milioni 545 Ikulu jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa na kulia ni Katibu Mkuu
wa Mambo ya Nje Balozi Dkt. Aziz Mlima.
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mfano wa hundi
hiyo mara baada ya kuipokea kutoka kwa Balozi wa India hapa nchini Sandeep Arya
aliyeiwasilisha kwa niaba ya Waziri Mkuu wa India Narendra Modi ili fedha hizo
zitumike kuwasaidia waathirika wa tetemeko mkoani Kagera.
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana na jambo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
mara baada ya kupokea msaada huo wa fedha kutoka Serikali ya India, Ikulu
jijini Dar es Salaam.
PICHA ZOTE NA IKULU







0 Comments