Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkurugenzi wa Hoteli ya Ramada
encore Abdul Ismail (kushoto),wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa Hoteli hiyo leo
Jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Samia Suluhu Hassan na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii
Meja Jenerali Mstaafu Gaudence Milanzi (kulia) wakiwa katika hafla ya uzinduzi
rasmi wa Hoteli hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Butiama Mhe.
Nimrod Mkono (kushoto) walipokutana katika hafla ya uzinduzi rasmi wa Hoteli ya
RAMADA encore leo Jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akielezea jambo wakati alipotembelea chumba
cha mazoezi kilichopo katika Hoteli ya RAMADA encore alipokuwa mgeni rasmi
katika uzinduzi wa Hoteli hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Msaidi wa
Msimamizi Msaidizi wa Mapokezi katika hoteli hiyo Bi. Janeth Leornard.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Samia Suluhu Hassan na Mkurugenzi wa Hoteli ya RAMADA encore, Abdul
Ismail (kulia) wakifurahia mara baada ya kuzindua rasmi Hoteli ya RAMADA encore
leo Jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Samia Suluhu Hassan( katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
viongozi waandamizi wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Uongozi wa Hoteli ya
RAMADA encore wakati wa hafla ya uzinduzi wa Hoteli hiyo leo Jijini Dar es
Salaam.
Picha na: Frank Shija, MAELEZO.






0 Comments