![]() |
| Daniel Zenda |
Na Mwandishi Wetu
................................
Shirikisho
la Vyuo vya Elimu ya Juu, limetoa pole kwa wale wote waliokumbwa na
kuathirika na maafa ya janga la tetemeko la ardhi yaliyotokea katika
mkoa wa Kagera, na baadhi ya sehemu za mikoa ya mwanza na Shinyanga.
Pamoja
na pole hizo, Shirikisho hilo, limempongeza Rais John Magufuli na
Serikali yake kwa jumla, kwa kuchukua hatua za haraka kwa kuonyesha
utayari na uharaka katika kuwasaidia walioathirika na janga hilo.
"Tungependa
kumpongeza kipekee, Mheshimiwa Rais kwa kuguswa na jambo hil, kiasi cha
kuamua kuahirisha ziara yake ya kiserikali ya siku tatu nchi Zambia,
ikiwemo kuhudhuria kuapishwa kwa Rais mpya wa Nchi hiyo", .
Hayo
yamesemwa leo jijini Dar es Salaam, na Mkuu wa Idara ya Mambo ya Nje na
Mahusiano ya Kitaifa na Kimataifa wa Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya
Juu, Katibu Msaidizi wa CCM, Daniel Zenda.
Amesema,
pia Shirkisho linawapongeza wadau na watanzania wote kwa jumla
waliojitokeza kwa haraka na wanaoendelea kujitokea hadi sasa kusaidia
kwa namna mbalimbali wanachi walioathiriwa na janga hilo la tetemeko la
ardhi, lililotokea Septemba 10, mwaka huu.
Zenda
amesema Shirikisho pia linatoa rai kwa wanasiasa kuacha kulitumia janga
hilo la tetemeko la ardhi kama fursa ya kujijenga na kutafuta umaarufu
wa kisiasa.
"Shirikisho
linawataka wanasiasa wakiwemo Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe,
Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi James Mbatia kuacha kutumia janga hilo
kuchonganisha wananchi na serkali yao ambayo imeshaanza kuchukua hatua
za muda mfupi na mrefu ikiwemo kuhakikisha waathirika wanapata makazi,
chakula na mali walizopoteza kutokana na janga hilo", alisema Zenda.
Zenda
ametoa mwito kwa walioathirika kuendelea kuwa na shubira kwa kuwa
serikali imeshaanza na inaendelea kuwa karibu nao katika kuhakikisha
hali yao inarejea katika mazingira bora kufuatia janga hilo ambalo
lilikuwa la dharura.

0 Comments