Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) Bw. Kailima Ramadhani akiwa kwenye studio za televisheni ya
Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) visiwani Zanzibar kutoa elimu ya mpiga
kura juzi.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(NEC) Bw. Kailima Ramadhani akifafanua jambo kwenye studio za televisheni ya
Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) visiwani Zanzibar wakati akitoa elimu ya
mpiga kura juzi.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) Bw. Kailima Ramadhani akifafanua jambo kwenye studio za
televisheni ya Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) visiwani Zanzibar wakati
akitoa elimu ya mpiga kura juzi.Kushoto ni muandaaji wa vipindi wa ZBC, Salha
Mohamed akiongoza kipindi cha Alasiri Yetu.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) Bw. Kailima Ramadhani, akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa ZBC
Iman Osmond (katikati) na Naibu MkurUgenzi Mkuu wa Shirika hilo Nasra Mohamed
baada ya kumaliza kipindi cha Alasiri Yetu, kutoa elimu ya mpiga kura.
Picha
na Hussein Makame,NEC
.................................................................................................
Hussein Makame, NEC
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inatarajia
kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura ifikapo mwaka wa fedha wa 2017/2018
kwa mara ya kwanza baada ya uchaguzi mkuu uliopita wa mwaka 2015.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC Bw.
Kailima Ramadhani wakati akitoa elimu ya mpiga kura kupitia kipindi cha Alasiri
Yetu kinachorushwa na televisheni ya Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC).
Alisema kuwa baada ya uboreshaji huo wa mwaka
2017/2018, Tume hiyo inategemea kuboresha kwa mara ya pili daftari hilo ifikapo
mwaka wa fedha 2019/2020.
Bw. Kailima alifafanua kuwa uboreshaji huo
unafanyika kwa mujibu wa kifungu namba 5 cha Sheria ya Tume ya Taifa ya
Uchaguzi kinachoielekeza NEC kuboresha daftari hilo mara mbili.
“Kwa mujibu wa kifungu namba 5 cha Sheria ya Tume
ya Taifa ya Uchaguzi kinasema Tume ya Taifa ya Uchaguzi itapaswa kuboresha
daftari la kudumu la wapiga kura mara mbili, baada ya uchaguzi mara moja na
kabla ya uchaguzi ujao mara moja” alisema Bw. Kailima na kuongeza kuwa:
“Kwa hiyo tumemaliza uchaguzi mwaka jana na kabla
ya uchaguzi wa mwaka 2020, Mungu akituweka hai tunategemea mwaka 2017/2018
tuboreshe daftari na mwaka 2019/2020 tufanye hivyo”
Mbali
na kuzungumzia uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, Bw. Kailima aleleza
jinsi tume hiyo inavyotekeleza mikakati ya kutoa elimu ya mpiga kura na kwamba
NEC itajipanga ili kwenda kutoa elimu hiyo visiwani Zanzibar.
Alisema NEC inapanga
kwenda kutoa elimu hiyo kwenye Chuo Kikuu Zanzibar (State University) mjini
Unguja na baadaye kwenda kisiwani Pemba na pia inategemea kushiriki Jitimai ili
kutoa elimu ya mpiga kura kwa washiriki wa mjumuiko huo.
Tume ya Taifa ya
Uchaguzi inaboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa lengo la kuandikisha
kila raia mwenye sifa za kupiga kura na kutunza taarifa zake katika Daftari la
Kudumu la Wapiga Kura.
Inaelezwa kuwa kuwepo
kwa Daftari sahihi la Wapiga Kura linaloaminiwa na wadau ni kigezo muhimu cha
kufanikisha chaguzi huru, wazi, zenye kukubalika na za haki zaidi.



