Random Posts

SERIKALI YARUHUSU WIMBO WA CHURA WA MSANII SNURA KUPIGWA

Msanii Snura Mushi (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imeruhusu kupigwa kwa wimbo wa chura ya kuufunga kwa kuwa haukuwa na maudhui mazuri ya kitanzania. Kushoto ni Msemaji wake, Baraka Nyagenda.
............................................................................................
Msanii wa bongo flaver snura mushi akubaliwa kuendelea kutumia wimbo wake wachura uliokuja na video mpya ukiachana na video ya awali iliyokuwa haina maadili ya kitanzania wimbo huu awali ulitangazwa kufungiwa tarehe 3/5/2016 na tarehe 5/5/2016 msanii huyu aliomba radhi kwa serikali na umma kwa ujumla.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Maisha Bezmet-makumbusholeo  amesema kuwa kwanza kabisa anamshukuru waziri Nape Nauye kwa kuruhusu wimbo wa chura ulioambatana na video mpya kurushwa, na kuonyeshwa katika vituo vya TV na Radio baada ya kuona wimbo huu kwa sasa umekuja na video yenye maadili ya kitanzania na sikupotosha maadili kama zamani.
“namsukuru mheshimiwa waziri Nape Nauye kwa kuruusu wimbowangu wa chura uliombatana na video mpya yenye maadili kurushwa katika televition na radio kama tulivyokuwa tumekubaliana awali kwamba wimbo wangu mpyua utafunguliwa endapo nitakuja na video mpya yenye maadili”
Kutokana na watu wengi kutoelewa maana halisi ya wimbo huo msanii huyo ameeleza nini ilikuwa maana na lengo la wimbo huo kwasababu awali watu wali imba wimbo na kutoa maana zao ambazo zilikuwa tofauti na matakwa yake hadi kupelekea wimbo uo kufungwa
“video yangu mpya ya chura unaeleza maana halisi ya neno chura niliyekuwa namzungumzia ikiwa na maana kwamba chura anaasili ya kurukaruka na huu wimbo na video imemfananisha chura na mwanamke asietulia katika mapenzi na kurukaruka na wanaume wengine linapotokea tatizo la mahusiana na kusababisha magonwa sugu na hii ndio maana halisi tofauti na watu walivyokuwa wakitafsiri”.

Pamoja na hayo ametoa shukrani zake kwa wizara ya habari , utamaduni,  sanaa na michezo, kwa elimu aliyopewa ambayo imempa mafunzo na kuahidi kutorudia kutoa wimbo na video isiyo kuwa na maadili  .na mpaka kufikia sasa wimbo wake wa chura ulioambatana na video mpya upo huru kurushwa ndani na ne ya nchi. 

Post a Comment

0 Comments