Mkuu
wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu akitoa taarifa kwa Waziri
wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kuhusu
hatua iliyofikiwa na serikali katika kurejesha hali baada ya tetemeko lilitokea
mkoani humo ambapo pia alimshukukuru Waziri Ummy kwa Misaada aliyoitoa wakati
wanakabiliana na maafa ikiwemo, Madawa, Vifaa tiba na madktari iliyowezesha
kusaidia kwa kiasi kikubwa waathirika wa tetemeko.
Waziri
wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea
na Mkuu wa Mkoa wa Kagera na kuipongeza kamati ya mkoa kwa namna walivyojipanga
kukabiliana na athari za tetemeko pamoja na kuwahudumia waathirika.
Waziri
wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimkabidhi
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu misaada iliyotolewa na
Bohari ya Madawa (MSD) waliotoa Dawa na Vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi
milioni 30.
Waziri
wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimkabidhi
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu mashuka 250
yaliyotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).
PICHA
NA ELEUTERI MANGI-MAELEZO



