Kocha Mkuu wa Mabingwa watetezi Yanga Hans Van Der Pluim.
..................................................................................
Na.Alex Mathias,Dar es salaam.
Kocha
Mkuu wa Mabingwa watetezi Yanga Hans Van Der Pluim,kuelekea mchezo wake
dhidi ya Ruvu Shooting majira ya saa kumi jioni ametangaza kikosi
kitakachoanza huku akiendelea kuwachunia walinda mlango wake na
kumuamini Kakolanya.
Mchezo
huu unatarajiwa kuchezwa katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam
huku wana jangwani hao wataingia na hasira na morali baada ya watani zao
Simba kufungwa jana na Prisons hivyo endapo watashinda watakuwa
wamebakiza pigo la pointi mbili hata wakifungwa watabaki nafasi hiyo
hiyo ya pili.
Kikosi cha Leo ni:Beno
Kakolanya,Hassani Kessy,Mwinyi Haji,Kelvin Yondani,Vicent Andrew,Thabani
Kamusoko,Haruna Niyonzima,Amis Tambwe,Donaldo Ngoma na Obrey Chirwa.
Wachezaji wa Akiba:Deogratius Munish,Oscar Joshua,Pato Ngonyani,Deus Kaseke,Anthony Mateo,Said Makapu na Juma Mahadhi.
Baada
ya kumalizika kwa mchezo huo Ligi itasimama na kusubiri raundi ya pili
ya mzunguko wa Vodacom Tanzania bara na kuanzia Novemba 15 timu zote
zitaanza usajili rasmi uliotangazwa na Shirikisho la mpira wa Miguu
Tanzania.
0 Comments