Winga wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Enock Atta Agyei,
akijaribu kuwatoka wachezaji wa Mtibwa Sugar, beki Salim Mbonde
(pembeni) na winga Kelvin Friday wakati wa mchezo wa kirafiki
uliofanyika usiku wa kuamkia leo ndani ya Uwanja wa Azam Complex,
Chamazi. Timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2.
Mshambuliaji wa Azam FC, Yahaya Mohammed, akijaribu kumtoka kiungo wa Mtibwa Sugar, Henry Joseph
Nahodha wa Azam FC, John Bocco, akiambaa na mpira mbele ya wachezaji wa Mtibwa Sugar
Winga wa Azam FC, Samuel Afful, akimkimbiza beki wa Mtibwa Sugar, Hassan Mganga.
Winga wa Azam FC, Joseph Mahundi, akitafuta maarifa ya kumtoka beki wa Mtibwa Sugar, Ally Shomari.





0 Comments